Na Mwandishi Wetu
DODOMA: BAADHI ya wazazi na walezi Mkoani Dodoma wamefurahishwa uanzishwaji wa sera mpya ya elimu ya mwaka 2024 toleo la kwaka 2014 kwa maelezo kuwa ni mkombozi kwa vijana wa Kitanzania.
Wakizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa nyakati tofauti wamesema uzinduzi wa sera hiyo inayolenga kuwapatia ujuzi itapunguza changamoto sugu ya ajira.
Mwanafunzi Fatuma Madida amesema serikali imeona kilio cha wazazi wengi kwa kuzindua mtaala huo mpya ulioboreshwa kwa lengo la kuwasaidia vijana wa kitanzania.

“Kama kweli sera hiyo itasimamiwa vizuri sina shaka kuwa vijana wengi watakuwa na ujuzi mkubwa na uzoefu wa kufanya kazi zao kwa kujiamini tofauti na sasa ambapo vijana wengo wanakosa kazi kwa kigezo cha kukosa uzoefu,” amesema.
Mzazi Titto Mwamalala amesema kitendo cha Serikali kuboresha mtaala ni kurejesha heshima ya elimu yenye ujuzi wa taaluma mbalimbali na kuingia katika ushindani wa ajira kimataifa na kitaifa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya New Precious Joseph Shinyanga, amesema kutokana na uboreshwaji wa mitaala shule hiyo pia itahakikisha inafanya vzuri kwani upatikanaji wa nyenzo kwa maana ya vitabu ni rahisi.

Katika kufanikisha ubora wa Elimu Mwalimu Shinyanga amewaomba wazaz, walezi pamoja na walimu kushirikiana kwa ukaribu zaidi na wanafunzi ili kuhakikisha ubora wa shule hiyo unaboeshwa.
Mkurugenzi wa Shule awali na msingi ya New Precious ,Justina William amesema kwa sasa elimu ya Tanzania inaenda kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania kwa kuwa na vijana wengi wenye taaluma na uzoefu.
Mkurugenzi huyo ambaye shule yake ipo Michese Jijini Dodoma amesema wamekuwa wakipokea wanafunzi tofauti tofauti wakiwepo wenye mahitaji maalumu.
“Shule yangu inapokea watoto wenye mahitaji Mbalimbali na kila mtoto analindwa kulingana na mahitaji yake hivyo wazazi na walezi wenye watoto wenye mahitaji muwalete hapa.
“Lakini pamoja na mambo mengine bado kuna changamoto mbalimbali kama vile miundombinu ya barabara hivyo tunamuomba Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuona uwezekano wa kusaidia kujenga barabara hata ya changalawe,” amesema.