MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wahitimu 3,561 wa Mafunzo Ya Huduma Za Afya Ngazi Ya Jamii,Wapatiwa Vitendea Kazi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wahitimu 3,561 wa Mafunzo Ya Huduma Za Afya Ngazi Ya Jamii,Wapatiwa Vitendea Kazi
Habari

Wahitimu 3,561 wa Mafunzo Ya Huduma Za Afya Ngazi Ya Jamii,Wapatiwa Vitendea Kazi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na  Mwandisi Wetu
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI kwa kushikiana na Wadau wa Sekta ya Afya imekabidhi seti ya vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya (WAJA) 3,561 waliohitimu mafunzo ya kutoa huduma za afya ngazi jamii.
Hayo yamejiri leo kupitia hafla fupi ya utoaji wa vyeti kwa wahitimu 222 katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, wakiwakilisha kundi la Wahudumu 3,561 awamu ya kwanza ya wahudumu waliohitimu mafunzo hayo katika mikoa 12.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Zuwena Jiri, akizungumza kwenye hafla hiyo amesema Serikali imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya karibu zaidi na wananchi na sasa tunashuhudia wahudumu hawa wa afya ngazi ya jamii wamehitimu na wapo tayari kwa ajili ya kuanza kazi wakiwa na nyenzo zote muhimu kwa ajili ya kufanya kazi kwa ufanisi.
“Mpango huu ulizinduliwa mwaka 2024 na Makamu wa Rais  Dkt. Phillip Isdor Mpango, hapo nyuma katika miaka 1970 tulikuwa na mpango huu pia lakini ulipitia changamoto za uratibu na awamu hii programu hii ya WAJA imeboreshwa zaidi ili kuleta tija zaidi katika kuimarisha huduma za kinga ndani ya jamii ili  kufikia lengo la Huduma za Afya kwa wote ifikapo mwaka 2030,” amesema Zuwena.
 Zuwena ameipongeza Serikali kwa kuweka mikakati endelevu ya kupatikana kwa WAJA wenye sifa stahiki na kuwaasa wahudumu hao wa afya kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na misingi ya utoaji huduma za afya.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema Wahudumu hao huchaguliwa na wananchi katika maeneo yao wanayoishi ambapo kila kitongoji au mtaa huchagua watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao Wizara huwapatia mafunzo ya darasani kwa muda wa miezi mitatu  na miezi mitatu mafunzo kwa vitendo katika jamii.
“Wahudumu hawa wa afya wako tayari kwa ajili ya kwenda kutoa huduma katika jamii, na leo hii Serikali inatoa vitendea kazi ikiwemo, sare, baiskeli, vishikwambi  vifaatiba ikiwemo vifaa vya kupimia shinikizo la damu, sukari, joto, uzito na vipeperushi vya elimu ya afya, yote haya ikiwa ni kuhakikisha mnakwenda kusaidia katika kuiamarisha huduma za kinga ndani ya jamii,” amesema Dkt. Magembe
Dkt. Magembe amesema Serikali imetoa vishikwambi hivyo kwa WAJA ili  vitumike katika kutunza na kutuma taarifa ambazo zitaunganishwa kwenye Mfumo wa taarifa za endeshaji wa Huduma za Afya (MTUHA) ambao kwa sasa taarifa zinawasilishwa kidigitali, hivyo kuifanya Serikali kuwa na taarifa sahihi zitakazosaidia katika kuboresha huduma za afya nchini.
Akizungumza kwa niaba ya WAJA  Dickson Maluchila ameishukuru Serikali pamoja na wadau wa Sekta ya Afya kwa kuwapatia mafunzo na vitendea kazi na kuahidi kuwa watakuwa mstari wa mbele katika kupunguza mzigo wa magonjwa na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za karibu na kwa wakati.

You Might Also Like

Maabara Ya Mkemia Mkuu Yashauri Wajasiriamali Wa Kemikali

Mkandarasi wa mradi wa REGROW, Kilolo  atakiwa kuongeza Kasi.

UDSM Yaipaisha Lugha Ya Kichina kwa Kuanzisha Digrii Ya Awali Ya Kichina, Kiingereza

Uwepo mwongozo kupima wagonjwa zaidi

Programu Ya Mazoezi Kwa Watumishi Wizara YA Mambo Ya Ndani Yazinduliwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Profesa Kitila Ataja Sababu Za Watanzania  Kumchagua Dkt Samia
Next Article FCC Yawavutia Wawekezaji Kwenye Maonesho Ya IATF Nchini Algeria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Habari October 28, 2025
Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri
Habari October 27, 2025
Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura
Habari October 25, 2025
Shibuda: WanaMaswa jitokezeni kupiga kura bila woga
Habari October 25, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?