MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi,waweke pingamizi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi,waweke pingamizi
Uncategorized

Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi,waweke pingamizi

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mohamed Mchengerwa amewataka wagombea wote ambao hawajaridhishwa na uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa waweke pingamizi ndani ya siku 2 kuanzia leo tarehe 08 – 09/11/2024.

Amesema hayo leo tarehe 8 .11.2024 wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu uteuzi wa wagombea katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

“Kama mnavyojua, leo ni siku muhimu ya uteuzi wa wagombea kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kanuni ya 18 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573, 574, pamoja na Kanuni ya 17 ya Tangazo la Serikali Na. 572 yote ya tarehe 12 Julai 2024.”

“Kanuni hizi zinamtaka Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kufanya uteuzi wa wagombea leo tarehe 8 Novemba, 2024, kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni. Mara baada ya uteuzi kukamilika, majina ya wagombea wenye sifa na wale ambao hawajakidhi vigezo vya kugombea yatabandikwa hadharani ili umma uweze kuyapata wakiwemo wagombea wenyewe”.Ameongeza Mchengerwa.

Ameendelea kueleza kuwa kwa mujibu wa Kanuni hizo mtu yeyote aliyeomba kuteuliwa kuwa mgombea au mgombea ambaye hakuridhika na uamuzi uliotolewa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, anaweza kuwasilisha pingamizi na kumuomba Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kupitia upya uamuzi uliofanyika ili amteue kuwa mgombea au atengue uteuzi anaoupinga.

Amesema kwamba pingamizi hili linaweza kuwasilishwa kwa maandishi ndani ya siku mbili tangu uamuzi au uteuzi ulipofanyika. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atalishughulikia pingamizi hilo na kutoa uamuzi ndani ya siku mbili tangu alipolipokea.

“Hivyo, kwa mujibu ya kanuni hizi, kuanzia leo tarehe 8 na kesho tarehe 9 Novemba 2024, kwa mgombea yeyote ambaye hatoridhika na uamuzi wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuhusu uteuzi, anapaswa kutumia nafasi ya siku hizi mbili ili malalamiko yake yaweze kufanyiwa kazi kwa mujibu wa Kanuni’.Amesisitiza

Amesema kwamba Uchaguzi huu unaongozwa na kanuni hivyo wagombea wasioridhika wanapaswa kuweka pingamizi na sio kuzungumza mitandaoni kwa sababu endapo utazungumza mitandaoni na hujawaweka pingamizi atakuwa hujafuata Kanuni hivyo wote wenye changamoto wahakikishe wanaweka pingamizi kwenye maeneo yao.

Ameongeza kuwa iwapo mgombea hatoridhika na uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi juu ya pingamizi lake, ana haki ya kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ndani ya muda usiozidi siku nne baada ya uamuzi huo kutolewa. Maana yake Rufaa ziwasilishwe kuanzia tarehe 10 hadi 13 Novemba, 2024 kwa kamati ya Rufaa.

Aidha, amesema ni muhimu wagombea wote wafuate taratibu za kisheria na kuhakikisha malalamiko yao yanawasilishwa katika sehemu sahihi ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi. Hii itasaidia kuimarisha utulivu na uwazi katika mchakato mzima wa uchaguzi.

You Might Also Like

GWSON yawakumbuka watoto wenye vichwa vikubwa,mgongo wazi kumbukizi ya Mwl.Nyerere

Waziri Pinda ashiriki mazishi ya Jaji Kipenka

Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki

Prof.Mwakalila azungumza na wanafunzi wapya wa MNMA asisitiza uadilifu na uzalendo

Wasira akipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  kwa kuenzi Falsafa za Baba wa Taifa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Prof.Mwakalila azungumza na wanafunzi wapya wa MNMA asisitiza uadilifu na uzalendo
Next Article
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?