Na Lucy Ngowi
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amewakumbusha wafanyakazi kujitokeza kupiga kura ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, viongoji na vijiji, Novemba 27 mwaka huu 2024.
Ridhiwani amewakumbusha hayo wafanyakazi alipokuwa akizindua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), jijini Dodoma.
“Sisi sote ni sehemu ya wanufaika wanaoshiriki katika uchaguzi huo, ni imani yangu wafanyakazi na familia zenu mliojiandikisha mtatumia vizuri nafasi hii kuchagua viongozi wa kutuongoza.
“Ninawaomba mjitokeze kwa wingi kuchagua viongozi siku itakapofika,” amesema Ridhiwani.