MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wadau wa Kisekta watakiwa kukabiliana na athari za mvua msimu 2024/25
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wadau wa Kisekta watakiwa kukabiliana na athari za mvua msimu 2024/25
Habari

Wadau wa Kisekta watakiwa kukabiliana na athari za mvua msimu 2024/25

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read
Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),  Jaji Mshibe Ali Bakari amewataka wadau kutoka sekta mbalimbali kukabialiana na athari zitakazoweza kujitokeza pamoja na kuchukua hatua stahiki wakati wa mvua za msimu zinatotarijwa kuanza mwezi Novembea 2024 hadi Aprili 2025 kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka hapa nchini.
Akizungumza hayo wakati akifungua rasmi mkutano wa nane wa wadau wa utabiri wa mvua za Msimu uliofanyika katika ukumbi wa PSSSF, Dodoma,alisema mvua za Msimu, Novemba 2023 hadi Aprili 2024 zilitawaliwa na uwepo wa hali ya El Niño. Hali hii ilisababisha uwepo wa matukio ya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini.
 “Napenda kutoa msisitizo kuwa, katika majadiliano ya mvua za Msimu ya mwaka huu, Novemba 2024 hadi Aprili 2025, tujikite katika kujadili athari zinazoweza kujitokeza na kutoa ushauri stahiki”. Amesema  Mshibe.
Jaji Mshibe amesema kuwa, Bodi itaendelea kuisimamia vizuri TMA katika utekelezaji wa mipango yake na kuiwezesha kutimiza ipasavyo Dira na mpango mkakati wake ili kuendelea kusaidia maendeleo ya nchi na Dunia kwa ujumla wake.
Aidha, amepongeza TMA kwa kuendelea kutoa utabiri wenye viwango vya juu vya usahihi unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Awali akizungumza Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Usimamizi wa Ubora TMA, Dkt. Geofrid Chikojo amesema mamlaka imeendelea kuboresha taarifa za hali ya hewa kwa kutoa utabiri mahususi kwa sekta mbalimbali, katika kuboresha taarifa hizo kwa wadau, TMA imeendelea kutoa taarifa za utabiri wa maeneo madogo kwa wilaya zote za mikoa iliyopo katika ukanda unaopata mvua za Msimu.
“Utabiri wa Wilaya 63 umeandaliwa kwa maeneo husika, hivyo ni vyema kila wilaya na kila sekta ikatumia taarifa hizo katika kufanya maamuzi na kuweka mipango ili kuboresha huduma zao kwa lengo la kuongeza tija na pia kupunguza madhara ya hali mbaya ya hewa yanapojitokeza”. Amesema  Dkt. Chikojo.
Naye mwakilishi wa wadau kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Cosmas Makomba ameeleza namna taarifa za awali za mvua za msimu 2023/24 zilivyosaidia katika kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuandaa mkakati wa maafa, kutoa mafunzo pamoja na kuandaa mpango wa dharura kwa mikoa iliyotarajiwa kuathirika.
Mkutano huu ni muendelezo wa sehemu ya ushirikishwaji wadau wakati wa maandalizi ya utabiri wa msimu husika ambapo wataalamu kutoka sekta mbalimbali, wanapatiwa fursa za kuona rasimu ya utabiri husika na kutoa michango yao juu ya athari zinazotarajiwa katika sekta husika pamoja na ushauri ili kuwezesha kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari hizo.
Aidha, TMA hutumia fursa hiyo kupokea mrejesho wa namna bora ya kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa nchini.

You Might Also Like

TRAWU yapigania mkataba hali bora za kazi miaka 11 sasa

LATRA CCC Yatoa Angalizo Uhitaji Mkubwa Wa Wasafiri Mwisho Wa Mwaka

Serikali kuleta kicheko kwa TASU 

CMA Inasaidia Vijana Kuwa Na Nafasi Bora Kazini

Afrika yatakiwa kutokuwa na Matabaka katika kutekeleza AFCFTA 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TFS Yawataka Wananchi Kufuga Nyuki Kuzuia Uharibifu Wa Mazingira
Next Article Samia Kalamu Award yasogeza Mbele
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?