MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waajiri Wathamini Taaluma Ya Uandishi Wa Habari – Dkt. Mkoko
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waajiri Wathamini Taaluma Ya Uandishi Wa Habari – Dkt. Mkoko
Habari

Waajiri Wathamini Taaluma Ya Uandishi Wa Habari – Dkt. Mkoko

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema kama vile Serikali inavyothamini taaluma ya Uandishi wa Habari na Waandishi wenyewe, ndivyo ambavyo waajiri ama wamiliki wa vyombo vya habari wanavyotakiwa kuwapa thamani wanayostahili.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha Upendo,  kwenye kipindi cha Wakeup Calls, Mjumbe wa Bodi hiyo Dkt. Egbert Mkoko amesema  kama Serikali inampa Mwandishi wa Habari Ithibati na Kitambulisho ina maana inamthamini.
“Serikali inamthamini huyu kwamba anastahili kuwa mwandishi wa habari kwa hiyo na yeye kama mwajiri ampe thamani inayostahili kwa sababu ukimwajiri halafu ukamwambia fanya kazi tutaangalia angalia mwisho mwa mwezi kama tutapata kitu, kama tukipata matangazo tutakupatia kitu, tusipopata tutaangalia mwezi ujao sasa hiyo itakuwa ajira au…,”
“Sasa hiyo inakuwa unaishushia hadhi taaluma yenyewe. Kwa hiyo kwanza tutapeana elimu licha ya kwamba tunajua kuwa vyombo vya habari uchumi haujakaa vizuri, na kuna ripoti ilitoka mwaka jana kuhusu hali ya uchumi wa vyombo vya habari nadhani kuna mambo yatafanyika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya vyombo vya habari kufanya kazi na kuwa na uchumi unaostahiki kuweza kuwalipa wana taaluma wake,” amesema.
Kwa mujibu wa Mjumbe huyo waandishi wa habari wanastahili kulipwa mishahara yao kwa wakati pia kupata haki zingine za msingi kama walivyo wafanyakazi wengine ikiwa ni pamoja na bima za afya.
“Na hilo ndilo moja ya jukumu lingine la bodi kuhakikisha ustawi wa waandishi wa habari katika vyombo vya habari wanavyofanyia kazi unazingatiwa na suala la afya ni la msingi sana kwani bila kuwa na afya njema huwezi kufanya lolote na kwamba ili uwe na uhakika wa afya njema ni muhimu kuwa na bima ya afya,” amesema.

You Might Also Like

UDSM Chasaini Mikataba Na Kampuni Za Kichina, Kujengea Uzoefu Wanafunzi Wake

Wanafunzi UDSM, MUM Kushiriki Fainali Ya Kimataifa Mashindano Ya Chinese Brigde

Chalamila Akabidhi milioni 100, saruji Kukamilisha Zahanati

Taasisi Za Serikali Zapewa Wiki Tano Kujiunga Na Mfumo

Mdau wa Maendeleo Goryo Ashinda Tuzo Ya Mlipa Kodi Bora

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article GST Yaelezea Mafanikio Yake
Next Article Dar Yaidhinishiwa Bil. 68 Ukarabati, Matengenezo Ya Barabara
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?