Na Lucy Ngowi
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), imetangaza fursa ya mafunzo ya udereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda.
Katika taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imeeleza kuwa, mafunzo hayo yatatolewa kwa gharama ya punguzo ya sh 30,000 kutoka sh 120,000 ya awali.
“Mafunzo yatakayotolewa ni usalama barabarani, matumizi ya vifaa kinga, udhibiti wa mwendo na matengenezo ya kawaida ya pikipiki , uendeshaji wa dharura na mbinu za kukabiliana na ajali .
” Sheria za udereva na usalama wa abiria, usimamizi wa kifedha na ujasiriamali,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa imetaja mikoa itakayotoa mafunzo hayo kuwa ni Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Manyara, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Tanga, Arusha na Kilimanjaro.
Mafunzo hayo yataanza Oktoba 20 mwaka huu katika vyuo mbalimbali katika mikoa husika.