MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: VETA Yatembelea Kiwanda Cha Kutengeneza Nyumba Bila Kutumia Tofali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > VETA Yatembelea Kiwanda Cha Kutengeneza Nyumba Bila Kutumia Tofali
Habari

VETA Yatembelea Kiwanda Cha Kutengeneza Nyumba Bila Kutumia Tofali

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WAFANYAKAZI kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wametembelea kiwanda cha COTWORLD, kujifunza kuhusu teknolojia mpya ya ujenzi wa nyumba za kisasa bila kutumia tofali.
Wafanyakazi hao ni kutoka VETA Makao Makuu na Kanda ya Dar es Salaam, waliongozana na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore katika  kiwanda hicho kilichopo Kigamboni.
Mkurugenzi Mkuu huyo Kasore amesema, lengo la kutembelea kiwanda hicho ni kuangalia namna VETA na COTWORLD wanavyoweza kushirikiana ili kuwezesha wanafunzi wa vyuo vya VETA kupata mafunzo ya vitendo kuhusu teknolojia hiyo.
Amesema teknolojia hiyo inahusisha matumizi ya chuma katika kusimamisha kuta badala ya tofali, mbinu inayolenga kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika sekta ya ujenzi.
 Amesema VETA inaendelea kuimarisha ushirikiano na viwanda ili kuhakikisha wanafunzi wake wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
“Tunahitaji kuwapa wanafunzi wetu maarifa na ujuzi wa kisasa ili waweze kushindana katika sekta ya ujenzi inayobadilika kwa kasi. Ushirikiano na viwanda kama COTWORLD ni hatua muhimu katika kufanikisha hili,” amesema.
Katika ziara hiyo, viongozi wa VETA walitembelea sehemu mbalimbali za kiwanda hicho na kushuhudia mchakato wa uzalishaji wa vifaa vya ujenzi vinavyotumika katika teknolojia hiyo mpya na kubaini fursa za mafunzo kwa wanafunzi wa VETA.
Baada ya ziara hiyo, pande zote mbili zimeahidi kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa vitendo katika ujenzi wa nyumba za kisasa.

You Might Also Like

Ufaulu Umeongezeka Kwenye Natokeo Kidato Cha Nne

Wadau wa Kisekta watakiwa kukabiliana na athari za mvua msimu 2024/25

Wakandarasi Miradi wa  TAZA Watakiwa Kukamilisha Kazi kwa Wakati 

Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025

CHAUMMA Yataka Kuvunja Bodi ya Korosho, Kuunda Mamlaka Mpya ya Mazao ya Kimkakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article ALAT Kujadili Ripoti Ya CAG
Next Article Kituo Cha Mkutano Cha Kimataifa Mlima Kilimanjaro Kuileta Dunia Tanzania
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?