Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) imesema inajivunia mageuzi makubwa iliyoyafanya katika sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini ambayo yamewezesha Watanzania wengi kujiajiri na kuajiriwa.
Mkurungezi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya kibiashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea.
Amesema VETA imekuwa ikitoa ujuzi katika maeneo ambayo yanawagusa watanzania kuweza kujiajiri na kuajiriwa katika sekta mbalimbali.
“Kwa sasa VETA tunatoa ujuzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa wale watu wanaohudumia wazee .majumbani , takribani watu 700 wameweza kuhitimu mafunzo na kupata ajira”amesema Kasore
Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kuweka msisitizo katika elimu ya mafunzo na Ufundi stadi .
Amesema kupitia msisitizo huo VETA wameweza kuona manufaa makubwa sana na kuweza kufaidika na kutekeleza mambo mengi .
“Kwa sasa VETA ina vyuo 80 nchini na 65 vinakwenda kumaliziwa na Serikali…Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi vyuo hivyo ambao upo katika hatua nzuri ya ukamilishaji wa awamu ya kwanza”amesema
Mkurungezi Mkuu huyo amesema kukamilika kwa vyuo hivyo VETA itakuwa na jumla 145 hapa nchini katika kila wilaya ambayo vinakwenda kuwasaidia wananchi kupata elimu na ujuzi wanaotaka Kwa urahisi.
Katika hatua nyingine Kasore amesema VETA imeanzisha Kampuni tanzu ambayo inahusuka na kukuza bidhaa bunifu zinazotegenezwa kupitia vyuo vyake mbalimbali .
Amesema bidhaa zote ambazo zitakuwa zikitegenezwa na wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo zitakuwa zikiuzwa katika Kampuni hiyo tanzu .
“Kampuni hii tanzu itakuwa ikihususika na bidhaa zote tunazozitegeneza pamoja na kutoa huduma mbalimbali kuanzia katika eneo la utengenezaji fanicha na usimamizi wa Miradi mbalimbali “amesema Kasore