Na Lucy Ngowi
DAr es Salaam: CHUO cha Ufundi Stadi (VETA), mkoani Mara wametengeneza mtambo unaochakata na kuchuja maji ya bwawa panapofugiwa samaki nje ya ziwa ama bahari.
Mwalimu wa wa Fani ya Bomba VETA Mara, Muhaji Ayub amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya miaka 30 ya uanzishwaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA), yanayoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mlutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam (JNICC).

Amesema wametengeneza mtambo huo kwa lengo la kuhamasisha ufugaji majumbani ama viwandani.
“Wazo hili limekuja baada ya Rais Samia Januari 30, mwaka jana 2024 alipokuja Mwanza kwenye hafla ya ugawaji vizimba kwa ajili ya kufugia samaki .
“VETA tukaona ni fursa kwetu, kuna kila sababu ya mtanzania kufanya ufugaji popote atakapotaka,” amesema.
Amesema mtambo huo unazunguka ili samaki apate hewa ya oksijeni . Pia mtambo unazalisha bacteria wa faida kwa sababu bakteria wa kwanza anachakata virutubisho zaidi kwenye maji.

“Bakteria wa pili anachakata kinyesi kinachozalishwa na samaki, kuhakikisha maji yanakuwa safi. Bacteria wa tatu anafanya uhamasishaji wa hewa nzuri ya oksijeni kwa samaki,” amesema.
Naye Mwanafunzi wa Fani ya Bomba, Jenipher John amesema elimu ya VETA imewasaidia wamepata uelewa wa ufugaji wa samaki.
“Nawashauri vijana mjiunge na VETA mjifunze ufugaji na utengenezaji wa mtambo,” amesema

Kwa uoande wake Msimamizi wa Maonyesho hayo, Faraja Mwampashe amesema VETA mkoani Mara wanashukuru kwa kushiriki jwenye maonesho hayo, wameweza kuonesha ubunifu wao wa kusaidia kuondoa uvuvi haramu ziwani au bandarini.