Na Lucy Lyatuu
CHUO Cha Mafunzo ya Ufundi Stadium VETA Dodoma wamebuni mashine inayorahisisha namna ya zao la alzeti linavyoweza kupekechuliwa kwa urahisi na kwa haraka.
Mkufunzi Wa VETA Dodoma, Hilary Nkwera amesema hayo wakati akizungumza na MFANYAKAZI katika Banda la VETA lililoko katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimaraifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema mashine hiyo ina uwezo Wa Kufanya kazi kwa saa sita bila kupumzuka na kuchakata alzeti gunia 30-35.
“Inatumia mfumo Wa injinibya peteoli kwa sababu mashamba mengi ya Wakulima Wa zao hili yako mje yaji na Ili kumrahisishia mkulima afanye kazi kwa ufanisi na kufikisha bidhaa yake sokoni kwa uhakika,” amesema.
Amesema asilimia kubwa ya Wakulima hupata Changamoto ya namna ya kupekechua alzeti ambapo mara nyingi hutumia fimbo kupigapiga zao hilo.
Nkwera anaiomba serikali kuongeza nguvu kwa VETA Ili vijana wengi waweze kuongeza Ujuzi ambao ni muhimu katika kuisaidia jamii.