Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: TANZANIA itaendelea kutoa ushirikiano katika kushughulikia mgogoro unaoendelea Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo pia akiwahakikishia wakuu wa nchi wa serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC).
Pia Rais Samia ametoa rai kwa jimuiya hizo mbili kuchukua hatua kuhakikisha kuwa DRC ambaye ni mwanachama wa EAC na SADC inakuwa salama na mgogoro unaoendelea hapa nchini.
Naye Rais wa Kenya, ambaye ni Mwenyekiti wa EAC, William Rutto amesema mgogoro huo unaendelea, hautamalizwa kwa kutumia silaha bali njia ya kidiplomasi