MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ufanisi Wa TANESCO Katika  Utekelezaji Na Usimamizi Wa Miradi Umeleta Mfumo Madhubuti Wa Nishati- Ndejembi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ufanisi Wa TANESCO Katika  Utekelezaji Na Usimamizi Wa Miradi Umeleta Mfumo Madhubuti Wa Nishati- Ndejembi
Habari

Ufanisi Wa TANESCO Katika  Utekelezaji Na Usimamizi Wa Miradi Umeleta Mfumo Madhubuti Wa Nishati- Ndejembi

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa Nishati,  Deogratius Ndejembi, amesema  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ya uzalishaji, usafirishaji na uambazaji wa umeme kwa ufanisi mkubwa, hatua inayoliwezesha taifa kusonga mbele katika kujenga mfumo madhubuti wa upatikanaji wa nishati ya umeme.

 

Ndejembi amesema hayo , wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma, ambapo ametaka kuona kazi inakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.

 

Ndejembi amebainisha kuwa mradi huo mkubwa unatekelezwa kwa fedha za ndani, na hadi kukamilika kwake utagharimu takribani sh bilioni 556.

 

“Niwaagize TANESCO kuendelea kumsimamia Mkandarasi kuhakikisha kazi inakamilika kulingana na ratiba. Hatutaki kufika mwisho wa utekelezaji na kukuta mradi umekabidhiwa bila kukamilika,” amesisitiza Waziri Ndejembi.

Habari Picha 10469

 

Ameongeza kuwa TANESCO imeelekezwa kukutana na Mkandarasi ili kuandaa mpango kazi mpya utakaoonesha mikakati ya ufuatiliaji wa hatua kwa hatua katika ukamilishaji wa mradi huo muhimu kwa taifa.

 

Aidha, Waziri Ndejembi amesema kuwa Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatoa msukumo mkubwa kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kote nchini kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Lazaro Twange, amesema Tanzania ina umeme wa kutosha kutoka kwenye vyanzo vyake vya uzalishaji, na kazi kubwa inayoendelea sasa ni kuutoa umeme huo katika maeneo ya uzalishaji na kuufikisha kwa wananchi na wawekezaji.

 

Twange ameeleza kuwa Serikali imekamilisha ujenzi wa vituo vikubwa vya kupokea na kupoza umeme katika Dodoma na Chalinze, ambavyo vitakuwa kitovu cha kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) na vyanzo vingine kwenda maeneo mbalimbali ya nchi.

Habari Picha 10470

 

“Kituo cha kupokea umeme cha Dodoma ni njia panda muhimu inayopokea umeme kutoka maeneo mbalimbali, na pia ndicho kinachotuunganisha na wenzetu nchini Kenya,” amesema  Twange

Habari Picha 10471

 

Ameongeza kuwa hatua hizi zote ni muhimu katika kulifanya taifa kuwa na mfumo imara wa umeme unaokidhi mahitaji ya sasa na ya vizazi vijavyo.

 

You Might Also Like

Wanaodaiwa Kumuua Ofisa TRA Washikiliwa na Polisi

TPHPA, KEM Wasaini Hati Ya Makubaliano Udhibiti Viuatilifu

RAAWU yapokea migogoro 16, yaishughulikia

TRC Yawatoa Hofu Wasafirishaji Mizigo Kwa Malori

BRELA kuanza kuwasajili wakulima

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NIDA Yapata Kibali Maalum Kurekebisha Taarifa Kwa Walioghushi Ili  Kujisajili
Next Article Kikwete Awahimiza Wahitimu wa UDSM Kuwa Mabalozi Wazuri wa Chuo 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Msama Aipongeza Hotuba Ya Samia, Atoa Neno Kwa Vijana, Wazee, Wanaharakati
Habari December 4, 2025
Profesa Silayo Aaga, Jawara Kuchukua Uongozi Mpya wa AFWC25
Habari December 3, 2025
Mpango Wa Taifa Wa Teknolojia Uko Mbioni Kuja-Serikali
Habari December 3, 2025
Petroli Yaendelea Kushuka Bei Desemba
Habari December 3, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?