Na Danson Kaijage
Dodoma: ILI kuwa na taifa lenye watu bora kimaadili na kiuchumi, ni vema kutumia mitandao kwa matumizi yenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jones Kilimbe, amesema hayo
wakati wa Maadhimisho ya siku ya Usalama Mtandaoni 2025 yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walimu wa shule ya msingi,vyuo vya kati na vyuo vya elimu ya juu.
Amesema kwa sasa kuna urahisi mkubwa matumìzi ya kimtandao pamoja na hasara kubwa iwapo mitandao itatumiwa vibaya.
Kwa upande mwingine amewataka wanafunzi kutoogopa masomo ya sayansi na hesabu kwa kuwa siyo magumu kama inavyoelezeka.
“Ninyi wanafunzi mnaosoma msiogope masomo ya Sayansi na hesabu kwani ni masomo pekee ambayo yanafanana duniani kote hivyo hayabadiliki na unaweza kuyapata mahali popote na kukufanya kuajiriwa mahali popote,” amesema.
Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka TCRA, John Daffa amesema siku ya usalama mtandaoni huadhimishwa Jumanne ya pili ya Februari kila mwaka ambayo ni mpango wa kimataifa ulioanzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuhamasisha matumizi sahihi na salama ya mtandao wa intaneti.
“Siku hii inasheherekewa takribani katika nchi 190 duniani,vilevile maadhimisho haya yanaunganisha mabilioni ya watu ulimwenguni kuhamasisha matumizi sahihi na salama mtandaoni, kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mtambuka mtandaoni haya miongoni mwa fursa yanayotokana na matumizi hayo,
Kwa upande wake mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Janeth Butashobya amesema kuwa utumiaji wa mitandao kwa sasa umestawisha upatikanaji wa nyenzo mbalimbali za kusaidia kujisomea.
Pia amesema kuwa upatikanaji wa mitandao kwa maana ya matumizi ya Intaneti kumerahisisha upatikanaji wa huduma muhimu na kupunguza matumizi matumizi ya muda.