Na Lucy Ngowi
DODOMA: HIFADHI za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania, inaunga mkono Jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha utalii.
Ofisa Masoko wa Hifadhi hiyo, Halima Tosiri amesema hayo katika Maonesho ya Wakulima Wafugaji na Wavuvi yaliyomalizika jana Agosti 10, 2024 katika viwanja vya Nzuguni Dodoma.
“Katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha utalii na kufikia malengo kuwa ikifika mwaka 2026, Tanzania yote kufikiwa na watalii milioni tano, nasi hatuko nyuma katika kuunga mkoni, jitihada hizo kwa kuhamasisha kufanya utalii katika maeneo ya bahari.
“Tunachukua fursa hii kuwakaribisha watanzania wote kutembelea katika maeneo yetu, wataweza kufanya shughuli mbalimbali za utalii, kwa kuogelea, kushuhudia magofu ya Kale ya kuanzia karne ya 13.
“Lakini pia kuna jamii mbalimbali za kasa, bustani ya matumbawe, lakini Mtwara tuna nyangumi wanaohama, lakini pia tuna bwawa lenye viboko, tuna fukwe nzuri zenye mhanga safi, lakini pia una vinjari kwa kutumia boti lakini pia kutembea katika njia za misiru,” amesema.