MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TUICO Arusha Yapongezwa Na AUWSA
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TUICO Arusha Yapongezwa Na AUWSA
Habari

TUICO Arusha Yapongezwa Na AUWSA

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Mwandishi Wetu

CHAMA  cha Wafanyakazi Wa Viwanda, Biashara, Taasisi Za Fedha, Huduma Na Ushauri (TUICO) Mkoa wa Arusha kimepongezwa na Menejimenti Mamlaka ya Maji Safi na Taka Mkoa wa Arusha (AUWSA),  kwa uamuzi wake wa kutoa mafunzo juu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF pamoja na mfuko wa hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa umma (PSSSF), kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka Jiji la Arusha (AUWSA), Kazimil Kanyanza aliwataka wafanyakazi kufuatilia kwa karibu mafunzo hayo ili kupata elimu sahihi kuhusiana na stahiki zao.

“Nyakati kama hizi za mafunzo ndio za kupata elimu sahihi kuhusiana na stahiki zako, lakini hata kujua zile fomula za kikokotoo, kuulizia mambo ambayo huyajui ili ujue na kujiandaa kuwekeza kabla ya kustaafu, isije ikatokea miaka miwili au mitatu baada ya kustaafu ukajikuta umetangulia mbele za haki kwa kuwa hukuwa umejiandaa,”amesema.

 

 

Amewataka wafanyakazi kutochagua viongozi wanaoenda kupambana na kuanzisha mgogoro na menejimenti badala yake wachague viongozi wenye ushawishi na uwezo wa kuwasilisha hoja zenye maslahi mapana kwa wafanyakazi ambazo zitakubalika na pande zote.

Hata hivyo amesema viongozi wa tawi la TUICO katika Mamlaka hiyo wamekuwa wakitekeleza majukumu yao vizuri kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wafanyakazi ambao ni wanachama wao na kutoa wito kwa viongozi watakaochaguliwa kuiga mfano wa viongozi wanaomaliza muda wao.

Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, Joseph  Shangali amewataka watumishi ambao ni wanachama wa chama cha wafanyakazi TUICO kote nchini kutumia mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa na watumishi wa TUICO kujua haki na stahiki zao wanazopaswa kuzipata kutoka kwa waajiri wao pamoja na kujiandaa vizuri kabla ya kustaafu.

Ametoa wito kwa wafanyakazi vijana wanaopata ajira mpya kote nchini kujiunga na chama cha wafanyakazi TUICO ili kuweza kutetewa, kulindwa kwa haki na maslahi yao pindi wanapopatwa na madhila kazini kupitia kwa waajiri wao.

Shangali amesema chama hicho Mkoa wa Arusha kimeandaa mafunzo hayo kwa wafanyakazi wa AUWSA kwa lengo la kuwapa ufahamu kuhusu mfuko wa hifadhi ya jamii (PSSSF), pamoja na mfuko wa fidia (WCF) ili kuweza kujua stahiki zao pale wanapoumia kazini na baada ya kustaafu utumishi wa umma.

“ Wafanyakazi wengi wanafanyakazi katika mazingira hatarishi ya kupata ajali lakini hawapati stahiki zao kwa kuwa hawajui kama kuna mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF), ambao unapaswa kuwafidia wanapopata majanga kazini, hivyo leo tumewaletea maofisa kutoka WCF ili waeleze wafanyakazi hawa namna mfuko wao unavyofanyakazi,”amesema.

Amesema  kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na kikokotoo hivyo wamelazimika kuwaita maofisa wa mfuko wa hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa umma (PSSSF), kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali kuhusiana na mafao kwa wafanyakazi ikiwemo kikokotoo.

Shangali amesema viongozi wa TUICO katika mamlaka hiyo wamemaliza muda wao hivyo mbali ya mafunzo pia watasimamia uchaguzi ili kupata viongozi wapya watakaoongoza kwa miaka mingine mitano kama katiba ya TUICO inavyoelekeza.

You Might Also Like

Mume na Mke Wafariki Kwa Wivu Wa Kimapenzi

Chuo Cha VETA Chazindua Mradi Wa Biogas

TANESCO Tunathamini Wadau Wa Maendeleo- Nyamo-Hanga

Miradi Ufungaji Mifumo Ya Umeme Jua 20,000 Mbioni Kuanza

TPHPA: Toeni taarifa mapema milipuko ya kwelea kwelea, nzige, viwavijeshi vamizi inapotokea

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TSLB Yatakiwa Kuimarisha Huduma za Kidijitali Ili Kukidhi Mahitaji ya Karne ya 21
Next Article Tanzania, Uturuki Zaweka Dira Mpya ya Biashara ya Dola Bil. Moja
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Benki Ya Dunia Kujenga Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa KV 400  Kutoka Uganda-Tanzania  
Habari July 23, 2025
Maliasili Yapongezwa Kwa Kutekeleza Maono Ya Rais Samia  
Habari July 23, 2025
Tanzania, Uturuki Zaweka Dira Mpya ya Biashara ya Dola Bil. Moja
Habari July 23, 2025
TSLB Yatakiwa Kuimarisha Huduma za Kidijitali Ili Kukidhi Mahitaji ya Karne ya 21
Habari July 23, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?