Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania TTCL limesema litatumia wiki ya huduma kwa wateja kuhakikisha miundombinu ya shirika inaboresha maisha ya Watanzania.
Kupitia Mpango Mkakati wa TTCL, tumejipanga kuhakikisha miundombinu yetuinaboresha maisha ya Watanzania. Tunaleta huduma bunifu, nafuu na zenye ubora wakimataifa, huku tukiweka ukaribu na wateja wetu katika kila hatua.

Akizindua wiki ya huduma kwa wateja kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo ,Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa TTCL Anita Moshi amesema shirika litahakikisha linaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake
“TTCL ni taasisi yenye maono ya kikanda na mchango mkubwa katika kukuza mawasiliano barani Afrika. Huduma zetu zimevuka mipaka ya Tanzania na kufika katikanchi jirani, jambo linaloifanya TTCL kuwa nguzo kuu ya mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,” amesema.
Ameongeza kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha huduma bora, za uhakika na zenye ubora wa kimataifa zinawafikia wateja wote wa ndani na nje ya Tanzania kupitia uwekezaji endelevu katika miundombinu ya kisasa na teknolojia za kisasa za mawasiliano.

“Tutakuwa wabunifu,wenye bidii na watumishi wenye maono yanayolenga matokeo kila mmoja wetu atakuwa sehemu ya suluhisho na kwa pamoja tutahakikisha kila mteja anathaminiwa,anasikilizwa na kuhudumiwa kwa ubora wa hali ya juu
“Hii ndio maana inayosukuma TTCL mbele kama taasisi ya mawasiliano yenye tija na dhamira thabiti,” amesema Moshi.
Amesema kupitia mpango mkakati wa TTCL watahakikisha miundombinu inaboresha maisha ya watanzania,kwa kuleta huduma bunifu ,nafuu na zenye ubora wa kimataifa huku ikiweka ukaribu na wateja kwa kila hatua.
Moshi amesema TTCL ni taasisi yenye maono ya kikanda na mchango mkubwa katika kukuza mawasiliano Barani Afrika.
“Tunatambua umuhimu mkubwa wa huduma zetu kwa wateja. Shirika linaendelea kutekeleza mpango wa upanuzi wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo kueneza Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hadi kufikiawilaya zote za Tanzania,” amesema

“Huduma zetu zimevuka mipaka ya Tanzania na kufika katika nchi jirani hivyo kutokana na hali hiyo tumejipanga kuhakikisha tunatoa huduma bora za uhakika zenye ubora wa kimataifa .
Aidha amesema shirika linatambua umuhimu wa huduma kwa wateja na litaendelea kutekeleza mpango wa upanuzi wa miundombinu ya mawasiliamo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kueneza mkongo wa taifa wa mawasiliano hadi kufikia wilaya zote nchini.
Amesema ujenzi wa minara 1,400 katika maeneo ya vijijini unaendelea kwa kasi ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano bila vikwazo sambamba na kuhakikisha huduma ya “faiba mlangoni kwako” inawafikia watanzania wote.
” Nawahakikishia wateja wetu wote kuwa TTCL tutaendelea kiwekeza katika teknolojia ya kisasa kuboresha mifumo na kuhakikisha huduma bora zinawafikia watanzania popote walipo”amesema Moshi.

Naye Mmoja wa wateja maalum aliyehudhuria uzinduzi huo,Mbarouk Seif amesema analiamini shirika hilo tangu lilipoanza kutoa huduma hadi sasa na kuwataka watanzania kutumia huduma zinazotolewa na TTCL ili waweze kupata huduma bora.