Na Mwandishi Wetu
MAREKANI: RAIS Mteule wa Marekani Donald Trump, tayari amemtangaza meneja wake wa kampeni Susan Summerall Wiles kuwa Mtendaji Mkuu Ikulu ya White House.
Trump ameweka wazi katika taarifa yake kwamba, Susan amemsaidia kuufikia ushindi mkubwa kisiasa alioupata katika historia ya nchi hiyo.