MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TRC Yawatoa Hofu Wasafirishaji Mizigo Kwa Malori
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TRC Yawatoa Hofu Wasafirishaji Mizigo Kwa Malori
Habari

TRC Yawatoa Hofu Wasafirishaji Mizigo Kwa Malori

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania(TRC), Masanja Kadogosa amewatoa hofu wafanyabiashara wakubwa wa usafirishaji mizigo kwa njia ya maroli kutokana na  ujio wa reli ya kisasa ya mizigo ya mwendo kasi kuwa reli hiyo haiwezi kuua biashara yao bali itawanufaisha zaidi wafanyabiashara na mlaji wa mwisho.
Kadogosa ameyasema alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio  ya miaka minne ya Shirika hilo katika kipindi cha  uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.
Kadogosa amezungumza hilo  baada ya mwandishi wa habari kuuliza swali juu ya kuwepo kwa wasiwasi inayotokana na wafanya biashara hususani wasafirishaji wa mizigo kwa kutumia maroli  kuwa uwepo wa reli hiyo inaweza kuua biashara ya wasafirishaji wa mizigo wanaotumia maroli.
Amesema  hakuna uhusiano wowote wa kuua biashara ya wafanyabiashara ya maroli bali ujio wa reli ya mwendo kasi ya kusafirisha mizigo itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wenyewe  na mlaji wa mwisho kwa kupata mzigo kwa haraka na kuusafirisha muda mfupi.
Akitolea mfano wa vifaa vya ujenzi amesema watu wa Dar es Salaam wanaweza kununua saruji mfuko mmoja kwa Sh. 15,000 hadi 16,000 lakini mtu wa Kanda ya Ziwa  ananunua kwa Sh.24000 hadi 26000 na hiyo inatokana na muda mrefu na gharama za njiani kwa njia ya barabara.
Amesema iwapo itatumika njia ya reli ya mwendo kasi itapunguza muda wa usafirishaji na gharama za njiani na kupelekea mnunuzi huyo kununua saruji kati ya Sh. 18000 hadi 20000 hivyo kujikuta anaokoa kati ya Sh. 4000 au 6000 jambo ambalo ni mafanikio makubwa kwa mlaji wa mwisho.
Mafanikio mengine ya Shirika hilo ni pamoja na utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia ya kuendeleza mradi huo na sasa umejumuisha, kipande cha Isaka – Mwanza, Makutopora-Tabora, Tabora – Isaka na kisha kumalizia vipande vya awamu ya pili kuelekea Kigoma.
Ameeleza Kadogosa kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani, ujenzi wa mradi wa SGR ulikuwa ukitekelezwa katika vipande viwili  vya Dar es salaam hadi Morogoro ambapo utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 83.55 na Morogoro hadi Makatupora ulikuwa umefikia asilimia  57.57.
“Mnamo Juni 2024, vipande hivi kutoka Dar es Salaam hadi Makutopora vyenye urefu wa kilometa 722 vimekamilika na kuanza kutoa huduma za usafirishaji wa abiria.
“Mafanikio makubwa ambayo Shirika kupitia serikali ni kuona umuhimu wa kuunganisha nchi za jirani kwa mtandao wa reli jambo ambalo limakuza uchumi zaidi na kuendelea kukuza mahusiano kato ya nchi ya Tanzania na nchi jirani,” amesema.

You Might Also Like

JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya

Kipaji pekee hakitoshi katika kufanya kazi za kihabari – Kipangula

Dkt. Mashimba Achukua Fomu Ya Kuwania Nafasi Ya Ubunge

Mauaji Yanayotokea Ni Aibu-Butiku

Wanafunzi, Watafiti, Wanataaluma Kujadili Dini, Utamaduni na Maisha ya Kisasa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania, Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana
Next Article Mwanjala Wa TRC Aelezea Umuhimu Wa VETA
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?