Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), kinapambana kupatikana kwa mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi mchakato ambao ulianza mwaka jana 2023 mpaka kufikia nwishoni mwa 2024 bado haujafanikiwa.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Eddo Makata amesema hayo alipozungumza na Mwandishi wa Mfanyakazi Tanzania,
Akizungumzia kuhusu mchakato huo waliouanza mwaka jana, amesema wana uhakika watafanikiwa kwa serikali kuwasikiliza.
“Mchakato ulianza tokea 2023 na mwaka huu tulifanya vikao na menejimenti ya TRC lakini jambo hilo halijakamilika,” amesema.

Amesema matumaini yao jambo hilo litakamilika mwaka 2025 kwa sababu serikali imeweka jicho katika suala la treni ya umeme ( SGR), huko inapeleka fedha nyingi katika ujenzi na uendeshaji wake.
” Kwa hiyo kwa serikali yetu hii Tuna uhakika kabisa haiwezi kuwa kimya isiweze kutilia maanani suala la mkataba wa hali bora, ambao ni wa. SGR ambao wanakuwa hawana mkataba wa hali bora.
” Tuna imani kabisa kupitia menejimenti ya TRC ambapo wafanyakazi wake wapo SGR na MGR mwaka 2025 tutaenda kukamilisha suala hili na mambo haya yatakuwa yamekamilika upande wa TRC,” amesema.
Pia amesema zipo nyaraka wataziangalia ambazo zina upungufu ikiwemo motisha kwa wafanyakazi wa TRC na staff regulations.
Pamoja na muundo wa mshahara kwa wafanyakazzi wa TRC.