Na Danson Kaijage
DODOMA: MAMLAKA ya Mapato Tanzania ( TRA), inafanya kazi kubwa ya kupambana na wafanyabiashara haramu wanaokwepa kodi kupitia bandari bubu.
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuh Mwenda amesema hayo alipokuwa anatoa taarifa ya maendeeo kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma juu ya mafanikio ya Mamaka hiyo kwa kiindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kutokana na kuwepo kwa bandari bubu wapo baadhi ya wafanya biashara ambao huingiza bidhaa kimagendo, wakati mwingine kuchepusha bidhaa badala ya kuvusha nje ya nchi kama vibali vinavyowataka na kurudisha bidhaa ndani.
Amesema TRA imejiimarisha zaidi katika kupambana na uhalifu huo na wale wanaobainika wanachukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kulipishwa faini.
Pia amesema ndani ya miaka minne Mamlaka hiyo imeweza kukusanya mapato kiasi cha Sh. Trilioni 21.2 sawa na asilimia 78.
Amesema kwa kipindi kama hicho kabla ya uongozi wa Rais Samia TRA ilikuwa na makusanyo ya Sh. Trilioni 11.12.
Amesema kuongezeka kwa mapato hayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuhimarisha mahusiano mema na wafanya biashara kwa kuboresha huduma kwa wafanyabiashara hao.