Na Lucy Ngowi
GEITA: WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS), imesema inazalisha mazao bora ya nyuki na kuwataka wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi kushiriki katika shughuli za ufugaji nyuki badala ya kuendeleza ukataji miti holela.
Mhifadhi Mwandamizi kutoka Shamba la Miti Silayo TFS , Juma Mdoe amesema hayo katika maonesho ya nane ya sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Mama Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita,

“Tunawahamasisha wananchi na wadau kuwekeza katika ufugaji nyuki kwa kuwa ni shughuli endelevu inayoongeza kipato bila kuharibu mazingira.
“Pia kuna fursa za utalii na michezo ya kimazingira kama mbio za nyika katika Shamba la Miti Silayo na Rubare,” amesema.

TFS, kupitia vitengo vyake ikiwemo Kituo cha Mbegu za Miti Morogoro na mashamba ya miti kama Silayo, inabaki mstari wa mbele katika kutoa elimu na kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali misitu nchini.