MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TEA Yakabidhi Miradi Iliyokamilika Wilayani Mtama, Masasi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TEA Yakabidhi Miradi Iliyokamilika Wilayani Mtama, Masasi
Habari

TEA Yakabidhi Miradi Iliyokamilika Wilayani Mtama, Masasi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SHULE tatu zilizonufaika na miradi ya Mfuko wa Elimu wa Taifa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake katika Halmashauri za Wilaya ya Mtama mkoani Lindi na Masasi (Mtwara), zimekabidhiwa vyeti.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Leonard Akwilapo amekabidhi vyeti hivyo kama ishara ya kuwakabidhi rasmi miradi hiyo kwa ajili ya matumizi na usimamizi.
Dkt. Akwilapo amekabidhi vyeti hivyo
wakati wa ziara yake ya kikazi kwenye halmashauri hizo. Pia amekagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na TEA kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa.
Akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi, James Chitumbe, Dkt. Akwilapo amesema ameridhishwa na ubora wa miradi iliyokamilika.
“Katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, nitakabidhi cheti kwa ajili ya mradi wa nyumba nne za walimu katika Shule ya Sekondari Lupaso, ambayo pia ina mradi mwingine wa jengo la utawala ambalo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 80,” amesema.
Vile vile katika Wilaya ya Mtama, amekabidhi vyeti kwa miradi ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Songambele na bweni moja la wanafunzi lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 katika Shule ya Sekondari Mnara, ambalo limekamilika kwa asilimia 100.
Kwa niaba ya wanufaika wa miradi hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Chitumbe, ameishukuru TEA kwa kufadhili miradi hiyo, akisema imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya elimu katika shule husika.
Mbali na kukabidhi miradi hiyo iliyokamilika, Dkt. Akwilapo pia alitembelea miradi mingine inayoendelea kutekelezwa, ikiwemo ujenzi wa maabara ya sayansi na nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari Ngongo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.

You Might Also Like

Ulega Ataka Ushirikiano Miradi Ya Kimkakati Ikamilike Kwa Wakati

CMA Inasaidia Vijana Kuwa Na Nafasi Bora Kazini

TARURA yaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa kujenga madaraja ya mawe

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

TPHPA Tuna Mchango Mkubwa Katika Utoshelevu Wa Chakula – Ndunguru

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika
Next Article Polisi Kufuatilia Wanaochuja Mafuta Na Mifuko Kwenye Malori
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TUICO Arusha Yapongezwa Na AUWSA
Habari July 23, 2025
TSLB Yatakiwa Kuimarisha Huduma za Kidijitali Ili Kukidhi Mahitaji ya Karne ya 21
Habari July 23, 2025
Tanzania, Belarus Zaanza Ukurasa Mpya wa Ushirikiano wa Kimkakati
Habari July 23, 2025
Rais Samia Atoa Bil. Nne Ujenzi Kiwanda Cha Kuzalisha  Nishati Mbadala  
Habari July 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?