Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma katika Maonyesho ya Kwanza ya Mfuko wa Utamaduni yaliyofanyika
mkoani Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi ndiye alitoa tuzo hizo, na kupongeza taasisi zote zilizoshiriki kwa mchango wao katika kufanikisha maonyesho hayo.
Mamlaka hiyo imekuwa miongoni mwa taasisi zaidi ya 30 zilizoshiriki katika maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni, kwa lengo la kuhamasisha na kuendeleza shughuli za kitamaduni nchini.

Vigezo vilivyotumika katika kutoa tuzo hizo ni pamoja na muonekano wa banda, utoaji wa huduma kwa wageni waliotembelea banda, pamoja na muda wa kufungua na kufunga huduma.
Maonyesho hayo yalianza Aprili 24 hadi 30, 2025 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.