MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TASAC yahadharisha wavuvi, wasafirishaji majini kuhusu upepo mkali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TASAC yahadharisha wavuvi, wasafirishaji majini kuhusu upepo mkali
Habari

TASAC yahadharisha wavuvi, wasafirishaji majini kuhusu upepo mkali

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limetoa tahadhari kwa wadau wote wa usafiri kwa njia ya maji, na wanaofanya shughuli za kiuchumi baharini na kwenye maziwa, kuchukua tahadhari kutokana na kuwepo kwa upepo mkali kwa siku tatu mfululizo kuanzia jana hadi kesho.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu TASAC, imetoa tahadhari hiyo baada ya kupokea taarifa ya upepo huo kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA).
Kwa mujibu wa taarifa ya TASAC, TMA imeeleza kuwa kuna uwezekano upepo huo mkali unaozidi kilomita 40 kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba mosi hadi tatu mwaka huu.
Maeneo yatakayoathiriwa ni yale ya Ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, baadhi ya maeneo ya Kusini mwa Ziwa Tanganyika katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Pia maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani ikijumuishwa Visiwa vya Mafia pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa imetaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni kuathitlrika na kughairishwa kwa baadhi ya shughuli za baharini na kuharibika kwa miundombinu ya bahari.
TASAC inawataka wadau wake hao kuchukua tahadhari hiyo mpaka TMA itakapotangaza hali ya hewa kuwa shwari ili kuzuia ajali zitakazohatarisha maisha ya wavuvi na wasafiri.

You Might Also Like

TARURA Yatenga Milioni 580 Kuboresha Barabara Zinazohudumia Sekta ya Madini Geita

Vyuo vya Kilimo vishirikishwe mradi wa BBT

Waratibu Wa Kitaifa Wa Nchi Za Jumuiya Ya Ukanda Wa Maziwa Makuu Wakutana Kinshasa

BOT Yatoa Elimu ya Uwekezaji, Fedha Kwa Wananchi Maonyesho ya Madini Geita

Mkurugenzi VETA Kasore Akiteta Jambo Na Mhitimu Fani Ya Ushonaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dkt. Biteko ashiriki kilele cha miaka 60 JWTZ
Next Article Shirikianeni kutekeleza majukumu- Possi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?