MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania yang’ara miradi ya Kinywe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Tanzania yang’ara miradi ya Kinywe
Uncategorized

Tanzania yang’ara miradi ya Kinywe

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read

Na Mwandishi wetu

Ripoti ya Benki ya Dunia na Takwimu za Taasisi ya Jiolojia ya Marekani kuhusu makisio ya utajiri wa mashapo ya Madini ya Kinywe ifikapo mwaka 2050 imeitaja nchi ya Tanzania kushika nafasi ya Sita (6) Duniani na nafasi ya Tatu (3) Afrika huku Msumbiji ikishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Madagasca kwa upande wa nchi za Afrika.

Hayo yamebainishwa Novemba 7, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance wakati akimwakilisha Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde katika mjadala wa Mawaziri ‘Ministerial session’ uliofanyika katika Kilele cha Mkutano wa Madini Muhimu Afrika uliofanyika Cape Town, Afrika Kusini na kuongeza kwamba, Tanzania imebarikiwa kuwa na aina nyingi za madini muhimu yanayohitajika kwa ajili ya uzalishaji wa nishati na teknolojia za kisasa.

Amesema Tanzania imejipanga katika ugunduzi wa madini ya kinywe na madini mengine ya nishati safi kama nikeli, Cobalt, lithium, rare earth elements na nobium kwa kuwa na taarifa za kutosha za kijilojia.

‘’Tanzania imeanza kutekeleza Madini Vision2030 yenye lengo la kupunguza uwezekano wa wawekezaji kupata hasara kwa kufanya tafiti maeneo ambayo hayana taarifa za kijilojia ‘derisking the sector’. Lengo la mkakati huo ni kufanya utafutaji wa madini kwa njia ya ndege (High Resolution Airbone Survey) kutoka asilimia 16 ya sasa na kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030’’

Dkt. Mwasse ameeleza kuwa ni muhimu sasa kwa nchi za Afrika kuwa na ushirikiano wa kuongeza thamani madini muhimu kwa kuweka viwanda katika nchi ambayo itakuwa inafaa kwa nchi nyingine za afrika. “Ni wakati mwafaka wa nchi za Afrika kufanya uchambuzi wa faida na hasara ‘cost benefit analysis” kuona sehemu sahihi ya kuweka mitambo ya kusafisha na kuongeza thamani madini muhimu” aliongeza “mfano kiwanda kitakachojengwa cha Kabanga Nickel multi-metal smelter cha kahama kitawezesha nchi jirani kama Burundi na Congo kusafisha madini yao pale ili wananchi wawe na ustawi kutokana na rasilimali za nchi yao na ilikufanikiwa katika jambo hili ni muhimu kuwa na ushirikiano baina ya nchi za Afrika,’’ amesisitiza Mwasse.

Ameongeza kwamba, Tanzania inaliimarisha Shirika lake la STAMICO ili kuvutia uwekezaji kwa kuwa na leseni zake ambazo inazifanyia utafiti kupunguza muda ambao mwekezaji anageutumia kuanza kufanya utafiti na uwezekano wa kupata hasara kwa kutokuwa na uhakika wa uwepo wa mashapo.

“Ni wakati mwafaka kwa nchi za Afrika kuimarisha Mashirika yao ya Madini yanayomilikiwa na nchi zao kuendeleza madini Muhimu na kuongeza manufaa ya nchi,’’ amesema.

You Might Also Like

Prof.Mwakalila azungumza na wanafunzi wapya wa MNMA asisitiza uadilifu na uzalendo

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Vinasaba 524 Vimepimwa Kwa Mkemia Mkuu

Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki

Bandari ya Kilwa kuleta mapinduzi sekta ya uvuvi nchini

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Trump Amteua Mtendaji Mkuu White House, Safari Ya Kuunda Timu Yake
Next Article Vipaumbele Vilivyopo Kwenye Mpango Wa Maendeleo Vitafsiriwe – Majaliwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?