TANZANIA kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) na Taasisi ya zinazoongoza katika mafunzo ya sekta ya ukarimu nchini Italia ( ENAIP) zimesaini hati ya makubaliano ikiwa ni mkakati mahsusi wa kuongeza ubora wa mafunzo kwa vitendo katika eneo la ukarimu na utalii nchini.
Makubaliano hayo yanatokana na maadhimisho ya wiki ya vyakula vya Kiitaliano duniani, ikiambatana na matukio mbalimbali nchini Tanzania.
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika jana Dar es salaam katika ukumbi wa ikishuhudiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana.
Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Chana amesema makubaliano hayo yamefikiwa baada ya maono yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutengeneza filamu ya Royal Tour kwa lengo la kuongeza wigo wa watalii nchini.
Amesema serikali ina mkakati wa kuongeza watalii kufikia mil tano ifikapo mwaka 2025 na kuongeza pato la Taifa kufikia dola za marekani bilioni sita kwa mwaka 2025.
Amesema pia kupitia filamu hiyo imejikita kuboresha huduma za kitalii na ndio maana NCT imeingia makubaliano na Taaisi ya ENAIP kwa lengo la kuongeza ujuzi, ufahamu wa vyakula n ahata lugha mbalimbali.
Amesema makubaliano hayo nimuhimu kwa Taifa kwa kuwa kwa sasa Utalii unachangia asilimia 17 ya pato la Taifa huku ikiingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25 huku shilingi ya Tanzania ikiendelea kuimarika.
Waziri Pindi amesema makubaliano hayo ni muhimu kwa taifa ambapo yatawajengea uwezo walimu,wanafunzi na menejimenti ya NCT katika kupika vyakula mbalimbali, lugha,suala la ukarimu kwa wageni na utalii.
“Kipaumbele chetu ni kuongeza idadi ya watalii kutoka mataifa yote duniani ikiwemo soko la Italia hivyo makubaliano hay ani mojawapo ya mkakati wa kutoa huduma bora kwa watalii hatimaye kuongeza idadi ya watalii nchini,”amesema.
Naye Mkuu wa NCT, Dk Florian Mtey amesema kuwa makubaliano hayo yatasaidia katika ukuzaji na utekelezaji wa mitaala katika Nyanja za ukarimu na utalii, kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu za kufundisha ukarimu na usimamizi wa vyuo vya utalii na ukarimu
“Juhudi hizi za ushirikiano zitaimarisha kwa kiasi kikubwa utoaji wa mafunzo katika sekta ya utalii na ukarimu na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta hiyo ambayo inabakia kuwa kipaumbele katika uchumi wan chi yetu”,amesema.
Aidha amesema makubaliano hayo yatasaidia katika kubadilishana uzoefu wa ubunifu na kusasisha teknoloji za ufundishaji na maabara kuongeza ujuzi katika ukarimu na utalii sambamba na kubadilishana uzoefu na ujuzi wa mbinu bora katika mafunzo ya kiufundi ya utalii na ukarimu
Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini Glussepe Sean Coppcla amesema kuwa kubadilishana uzoefu baina ya nchi hizo mbili ni muhimu katika kukuza sekta ya utalii ambayo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya Taifa
Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa ENAIP Veneto Impresa Sociate, Antonino Ziglio, Maofisa kutoka ubalozi wa italia nchini Tanzanaia, viongozi kutoka ENAIP na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara ya maliasili na utalii.
Maadhimisho ya msimu wa tisa wa wiki y a vyakula kiitaliano duniani yameanza Novemba 16-23,2024 na kwa Tanzania watashirikiana na migahawa kadhaa ya Kiitaliano kutoka Tanzania Bara na Visiwani Pamoja na wakala wa Biashara wa Italia (ITA) kuhamasisha vyakula vyenye madhari ya kiitaliano katika migahawa kutoka Dar es Salaam, Iringa, Arusha na maeneo mbalimbali Zanzibar.