Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetakiwa kuendeleza kasi ya utendaji mzuri katika Utekelezaji wa Miradi ya uzalishaji na Usambazaji Umeme nchini pamoja na suala zima la Utoaji.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema hayo leo mara baada ya kutembelea banda la TANESCO katika Mkutano wa 9 wa Wahandisi Wanawake kwa mwaka 2024.
Bashungwa ambaye ndiye mgeni rasmi katika maonesho hayo, ameelezea kufurahishwa kwake na hatua nzuri zilizofikiwa na TANESCO katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme nchini pamoja na suala zima la Uboreshaji wa utoaji huduma kwa watumiaji wa umeme.
Amesa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, Gissima Nyamo-Hanga, Watumishi walioshiriki Maonesho hayo wamepokea pongezi hizo na kuahidi kuzidisha kasi ya utendaji na utoaji wa Huduma bora kwa Wadau.
Mkutano huo wa Wahandisi Wanawake unakwenda pamoja na Maonesho yanayoshirikisha Taasisi Mbalimbali hapa nchini.