Na Danson Kaijage Dodoma.
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimeelezwa kitendo cha viongozi wa kisiasa kuwanyanyasa wafanyakazi na wakati mwingine kuwatolea maneno ya unyanyasaji.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa TALGWU Tumaini Nyamhokya alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Utumishi vijana na ajira Deu Sangu katika ufunguzi wa Kikao cha 31cha Baraza kuu la TALGWU Taifa kilichofanyika Jijini Dodoma.
Nyamhokya amesema kuwa imekuwa ikishusha molali ya utendaji kazi kwa watumishi ambao wanapokea maneno ya kero pale viongozi wa kisiasa wanapokuwa katika ziara za ukaguzi wa miradi.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hawataki kufanya vurugu ya aina yoyote wala kuingia barabarani badala yake wao wanaamini katika kukaa mezani na kufanya majadiliano kwa lengo la kumaliza migogoro.
“Tuwatake sasa wanasiasa kutumia lugha za Staha kwa wafanyakazi badala ya kutumia lugha za uzalilishaji kama kuwafokea hadharani kwa kuwaambia kuwa hawafai
“Sisi tukiwa wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa tunaamini katika kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kwa kuzingatia misingi ya sheria ya kazi na pale inapoonekana kuna tatizo basi zitumike njia sahihi za kuzungumza na watumishi wa Umma na siyo kuwazodoa hadharani na kuwadhalilisha kwenye vyombo vya habari”ameeleza Nyamhokya.





