MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TALGWU Taifa Yataja Kero Saba Kubwa za Watumishi wa Serikali za Mitaa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TALGWU Taifa Yataja Kero Saba Kubwa za Watumishi wa Serikali za Mitaa
Habari

TALGWU Taifa Yataja Kero Saba Kubwa za Watumishi wa Serikali za Mitaa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Taifa kimetaja changamoto saba kuu zinazowakabili watumishi wa umma, zikiwemo kucheleweshwa kwa malipo ya stahiki, mifumo ya kiutumishi na masuala ya heshima kazini.
Habari Picha 10799
Akisoma risala mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi), Deus Sangu, wakati wa ufunguzi wa kikao cha 31 cha Baraza Kuu la TALGWU Taifa jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Wandiba Ngocho, amesema changamoto kubwa ni kutolipwa kwa wakati fedha za likizo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Ameeeleza kuwa utaratibu wa kulipa fedha hizo kupitia mapato ya ndani ya halmashauri umesababisha watumishi wengi kucheleweshewa malipo, wengine tangu mwaka 2018.
TALGWU imeiomba Serikali itenge bajeti ya likizo kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali, kama ilivyo kwa watumishi wa kada ya ualimu.
Habari Picha 10802
Changamoto ya pili ni malipo ya leseni za kutoa huduma  kwa watumishi wa kada ya afya, ambapo wamekuwa wakilazimika kujilipia ada hizo binafsi.
TALGWU imependekeza waajiri walipe ada hizo na leseni hizo zisitumike kama kigezo cha kupandishwa madaraja.
Ngocho pia alilalamikia tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuwadhalilisha watumishi wa umma hadharani, hasa wakati wa ziara za ukaguzi wa miradi.
Alisema hatua hiyo hushusha morali ya kazi na kuharibu taswira ya utumishi wa umma, akisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za kisheria na kiutawala.
Habari Picha 10803
Changamoto nyingine ni kutolipwa kwa wakati stahiki za uhamisho, licha ya maelekezo ya Serikali kutowahamisha watumishi bila bajeti.
Aidha, TALGWU ilibainisha changamoto katika matumizi ya mfumo wa upimaji wa utendaji kazi (PEPMIS), ikiiomba Serikali kuongeza elimu kwa watumishi na wasimamizi wao.
Kwa upande wa miundo ya utumishi, chama kilieleza kuwepo kwa matatizo ya kubadilishiwa vyeo kwa kada zisizo za walimu, bila kuzingatia uzoefu wa mtumishi.
Pia kiliomba shahada ya uzamili iwe kigezo cha nafasi za uteuzi, si sharti la kimuundo.
Changamoto ya saba ni kutokuhuishwa kwa wakati Mabaraza ya Wafanyakazi, ambapo hadi Desemba 2025, mabaraza 60 kati ya 197 yatakuwa yameisha muda wake.
TALGWU imemuomba Waziri kuwaelekeza waajiri kutekeleza matakwa ya kisheria.

You Might Also Like

Sheikh wa Mkoa, ‘Wanaotoa Rushwa Msiwachague’

Rais Samia Ni Mama Wa Maendeleo – Majaliwa

Polisi Yaimarisha Usalama Timu za Simba na Yanga Kesho

Tanzania, Comoro Zaongeza Ushirikiano wa Lugha

MSD Yaokoa Zaidi Ya Mil. 15

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TALGWU Wakerwa Na Wanasiasa Kuwadhalilisha Watumishi Wa Umma
Next Article Jumuiya ya Wazazi CCM: Uchaguzi Ulikuwa Mgumu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?