Na Lucy Ngowi
SPIKA wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, ametangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, kilichotokea leo Desemba 11, 2025, Jijini Dodoma.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo tarehe 11 Desemba 2025, Jijini Dodoma,” amesema.
Ametoa pole kwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho, akiwataka kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
Amesema kuwa Ofisi ya Bunge, kwa kushirikiana na familia ya marehemu, inaendelea kuratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitatolewa kadri zitakapopatikana.
Marehemu Jenista Mhagama alizaliwa Juni 23, 1967 na amefariki dunia leo Desemba 11, 2025.

