MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Soko La Kisasa La Nyamachoma Lazinduliwa Vingunguti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Soko La Kisasa La Nyamachoma Lazinduliwa Vingunguti
Habari

Soko La Kisasa La Nyamachoma Lazinduliwa Vingunguti

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa   amezindua soko la kisasa la nyama choma la Kumbilamoto vingunguti, Ilala jijini Dar es Salaam na kushuhudia utiaji wa mikataba ya  miradi sita ya maendeleo  yenye  thamani ya  shilingi bilioni 7.7
Mara baada ya kuzindua soko hilo ambalo limegharimu takribani sh milioni 727 amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kufanikisha mradi huo ambapo amezitaka Halmashauri nyingine kuiga  mfano huo.
Aidha, amefafanua kuwa soko hilo litakwenda kuwapatia ajira  wananchi wengi huku akisisitiza  kuendelea kulitunza  ili lisiharibike kwenye kipindi kifupi.
Mchengerwa ameongeza kuwa kukamilika kwa soko hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na  kufafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita tayari imekamilisha  miradi  mingi kama iilivyoahidi.
Wakati  huo huo Waziri Mchengerwa amezitaka Halmashauri zote nchini kutimiza malengo  zilizojiwekea ya ukusanyaji  mapato ili  ziweze kutekeleza  miradi ya  maendeleo huku akizitaka  kuendelea kubuni miradi  mbalimbali ya maendeleo yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu wakandarasi wazawa, Mchengerwa  amezitaka Halmashauri na mikoa  yote nchini kuwapa kipaumbele  wakandarasi wazawa huku akitoa wito  kuwachukulia hatua wakandarasi wanaofanya  vibaya  katika  kazi wanazopewa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Edward Mpogole amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa  mikataba yote iliyosainiwa inakwenda kukamilika  kabla ya mwisho wa mwaka na kwamba wananchi watakwenda kunufaika  na miradi hiyo.
Katika uzinduzi wa soko hilo Naibu Spika  Mussa Zungu ambaye  pia ni Mbunge wa Ilala amewataka watanzania  kutojihusisha na uvunjaji wa amani   katika kipindi hiki  cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  Oktoba  mwaka  huu
 Amina Selemani ambaye  ni miongoni mwa mfanyabiashara  katika soko  hilo amemshukuru  Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za kujenga soko  hilo ambalo limetoa ajira  kwa akina mama wengi.
“Kwa kweli tunamshukuru Mheshimiwa Rais  wetu  kwa upendo huu wa kutuletea  mradi huu wa soko ambao  umekuwa ni ukombozi kwa  maisha yetu”. Amefafanua Amina

You Might Also Like

UDSM Chasaini Mikataba Na Kampuni Za Kichina, Kujengea Uzoefu Wanafunzi Wake

Michezo Yapunguza Uhalifu Dodoma

Rasmi Leo DSM Kuanza Biashara Saa 24

Ofisi Ya Mwandishi Mkuu Wa Sheria Yakamilisha Rasimu Ya Sheria 446 Kwa Lugha Ya Kiswahili

Wastaafu Epukeni Matapeli Kwenye Mafao-PSSSF

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article JAB Yatoa Mwezi Moja Kuthibitishwa, kupewa vitabulisho
Next Article CCM Kuwezesha Wananchi Kufuatilia Mkutano Mkuu Maeneo Ya Wazi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nyanya Cheri na Ngogwe Chungu Zarejea 
Habari July 13, 2025
NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje
Habari July 13, 2025
Kafulila: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma Kuboresha Huduma
Habari July 13, 2025
Teknolojia Mpya Ya Uchomeleaji Yaleta Mapinduzi VETA Dodoma
Habari July 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?