Na Danson Kaijage.
MKUU wa Mkoa Singida, Halima Dendegu amesema katika kipindi cha miaka minne mkoa wa Singida umepokea kiasi cha Sh. Trilion 1.72 kutoka serikali kuu,Mapato ya ndani na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali katika mkoa huo.
“Pato la Mkoa limeongezeka kutoka Sh. 2.709 Trilioni mwaka 2020/21 hadi Sh. Trilioni 3.398 mwaka 2024/25,wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja umeongezeka kutoka Tshs. 1,588,604.66 (2020/21) hadi Tshs. 1,710,562.00 mwaka 2024/25.

“Mkoa wa Singida kwa ujumla katika kipindi hiki umepokea jumla ya Trioni . 1.72 toka Serikali kuu, Mapato ya ndani na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kugharamia shughuli za uendeshaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ,Fedha zilizotoka Serikali kuu zikiwa Trioni 1.055,”amesema.
Aidha amesema katika kipindi hicho makusanyo ya ‘TRA’ yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 11.9 mwaka 2021/22 hadi shilingi Bilioni 30 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la 152% huku makusanyo ya mapato ya ndani yakiongezeka kutoka shilingi Bilioni 14.6 mwaka 2020/21 hadi shilingi Bilioni 24.8 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la 69.8%.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo amesema vituo vya kutolea huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali vimeongezeka kutoka vituo 203 mwaka 2020/21 haid vituo 302 mwaka 2024/25 huku Shule mpya za msingi 142,shule mpya za sekondari 40 ,shule mpya 7 za amali na vyuo vinne vya VETA vinajengwa katika kipindi cha miaka minne.
“Takribani Bilion 48 zimetumika kutoa elimu bila malipo utoaji wa vyakula mashuleni umefikia 95% Kupungua kwa utoro uimarishaji wa vyuo (Chuo cha utumishi wa umma na uhasibu) na sekta ya afya tumeongeza Zahanati kutoka 173 hadi 246,Vituo vya Afya vimeongezeka kutoka 25 hadi 42 na ujenzi wa Hospitali za Wilaya mpya 5 na ukarabati mkubwa 3,”amesema