MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Sierra Leone Yaipongeza TARURAUjenzi Wa Madaraja, Barabara Za Mawe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Sierra Leone Yaipongeza TARURAUjenzi Wa Madaraja, Barabara Za Mawe
Habari

Sierra Leone Yaipongeza TARURAUjenzi Wa Madaraja, Barabara Za Mawe

Author
By Author
Share
3 Min Read
TARURA Yasema Matumizi Ya Mawe hupunguza asilimia 40 ymYa Gharama
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Matengenezo ya Barabara wa Sierra Leone  Mohamed Kallon ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ujenzi wa madaraja na barabara kwa kutumia mawe.
Akizungumza na waandishi wa habari Mtendaji Mkuu huyo amesema wamefurahishwa na teknolojia hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inapunguza gharama za ujenzi pia kutumia malighafi zilizopo eneo husika.
Amesema kwamba ujio wao hapa nchini  ni kujifunza ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya katika maeneo ya mipango, ushirikishwaji wa wananchi na utumiaji wa teknolojia mbadala.
“Wananchi wa Sierra Leone ni wazalishaji na wengi wanaishi vijijini hivyo kwa kutumia teknolojia ya mawe itawarahisishia kusafirisha mazao yao kutoka mashambani kwenda kwenye masoko,” amesema.
Amesema  kati ya agenda tano za Rais wa nchi yao ni kuilisha Sierra Leone hivyo kitu muhimu ni kufungua barabara ili kuuza na kusafirisha mazao toka kwa wakulima.
Kwa upande wa ushirikishwaji wa wananchi  amesema wameona ni fursa nzuri kuja kujifunza Tanzania kwa sababu wao hawaitumii njia hiyo ya vikundi vya kijamii ila tayari TARURA wamefanikiwa katika utekelezaji wa miradi yao kwenye wilaya.
Naye, Mtendaji Mkuu wa TARURA  Victor Seff amesema kwamba matumizi ya malighafi za ujenzi wa barabara  kama mawe yaliyopo  kwenye eneo la kazi inapunguza gharama za ujenzi wa madaraja na barabara kwa zaidi ya asilimia 40.
Kwa upande kwa ushirikishwaji wa vikundi vya kijamii kwenye ujenzi na matengezo ya barabara Seff amesema kupitia mradi wa uboreshaji  wa barabara za vijijini ambao ni mkopo rahisi toka Benki ya dunia ambao wanasaidia kuanzisha, kufundisha na kuviwezesha vikundi hivyo kufanya kazi za matengenezo ya barabara kwa weledi na umakini.
“Faida kubwa ya kuvitumia vikundi hivyo inapunguza gharama kwani vinatoka maeneo  yale yale zinapopita barabara pia inasaidia kulinda miundombinu ya barabara ikiwemo alama za barabarani kwani wanatambua barabara ni mali yao”.
Hata hivyo Seff amesema  TARURA wapo tayari kushirikiana na Sierra Leone kwa kuwapatia wataalam wa kufundisha pale panapohitajika.
Timu ya Viongozi na wataalam kutoka Sierra Leone wapo nchini kwa ajili ya kujifunza ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya katika maeneo ya mipango, ushirikishwaji wa wananchi pamoja na teknolojia mbadala na wanatarajia kuvitembelea baadhi ya vikundi vya kijamii Mkoani Njombe.

You Might Also Like

  Tanesco Yagawa Zawadi Ya Majiko Sabasaba Kuhimiza Matumizi Nishati Safi

Watanzania Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii

Dar Yaidhinishiwa Bil. 68 Ukarabati, Matengenezo Ya Barabara

Samia Azindua Shule ya Msingi ya Mchepuko wa Kiingereza Songea

Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Kushirikiana na Finland Uboreshaji Mbegu za Miti
Next Article VETA yawafikia madereva ‘Boda boda’
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?