Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Semesi kwa utendaji na utekelezaji wa mikakati yenye kuleta tija katika suala zima la Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Nchi.
Profesa. Shemdoe amezitoa pongezi hizo alipotemblelea banda la NEMC katika maonesho ya wakulima ( Nanenane) yenye kaulimbiu isemayo ” Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi”.
Shemdoe pia ameelezwa mikakati endelevu yenye kuleta tija katika suala zima la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.
Profesa Shemdoe amesema ” NEMC mmepata kiongozi mzuri, ni mtendaji, mtekelezaji na mfuatiliaji wa mambo, hakika mazingira yapo salama chini ya NEMC,”