Na Danson Kaijage
DODOMA: SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma Alhaji Dkt. Mustapha Shaban Rajabu akemea baadhi ya wanawake wanaojipamba kinyume cha maagizo ya Mungu,
Pia wenye kuvaa nguo za kuonesha maumbile yao, kwa kusema kujipamba huko ni sawa na uchafu au kujipaka matope.
Sheikh Rajab amekemea hilo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya Eid ul-Fitr iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma.
Amesema kwa sasa wapo wanawake wameacha maadili ya Kimungu na kufanya mambo yao wenyewe hususani wakati wa kujipamba na kuvaa mavazi yasiyo na stara.
Amesema mwanamke ambaye anajibandika kope,nywele bandia, kujichubua kwa kujiongezea weupe, kuvaa nguo za aibu za kuonyesha maumbile ni sawa na kujipaka uchafu katika mwili, wawapo kwenye ibada hawawezi kupata thawabu.
“Katika dini ya Kiislamu sheria inaweka wazi kwa kumtaka mwanamke kuvaa nguo za kujisitiri mwili wake
“Kwa sheria hiyo mwanamke anapokuwa ajajisitiri vyema ni sawa kama yupo uchi kwa maana sehemu ambayo haihesabiki kuwa uchi kwa mwanamke ni usoni na viganja viwili vya mikono.
“Lakini iwapo ataacha kifua wazi,tumbo,kitovu au kuvaa nguo zinazoonesha maumbile yake huyo mtu ni sawa na aliye uchi kwa kuwa tayari sheria za dini ya Kiislamu zinamkataza,” amesema.
Amesema mwanamke anasitirika kwa kuvaa mavazi marefu na kuchora hina au piko, achorwe na mumeo, kuonwa na mumewe tu hayo maua.
Hata hivyo amesema sheria ya dini ya kiislamu inawazuia wanaume kuvaa mavazi ya kubana na kuonesha maumbile,kusuka nywele,kuvaa kikuku au kuvaa milegezo au namna yoyote ya mavazi yampasayo mwanamke.
Amesema mwaname wa aina hiyo ni machukizo mbele za Mungu na kwa kufanya hivyo dini ya kiislamu inamuona kama mwanaume huyo ni firauni.