MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaweka Mkazo Kukuza Tasnia Ya Ufugaji Wa Kuku
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaweka Mkazo Kukuza Tasnia Ya Ufugaji Wa Kuku
Habari

Serikali Yaweka Mkazo Kukuza Tasnia Ya Ufugaji Wa Kuku

Author
By Author
Share
4 Min Read
 Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema  ujio wa Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao kwa Nchi za Kusini mwa Afrika unadhihirisha  namna Tanzania  ilivyokuwa na mahusiano mazuri ambayo yamefungua milango katika sekta mbalimbali .
Amesema hayo leo Oktoba 16, 2024 jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Makamu wa Rais  Dkt. Philip Isdory Mpango katika ufunguzi wa mkutano huo.
Ametaja faida za ufugaji kuku na ndege wafugwao kuwa ni pamoja na kuchangia usalama wa chakula na kuongeza pato la Taifa kikanda na kimataifa.
Amesema kuwa asilimia 55 ya kaya nchini na katika nchi mbalimbali ni ufugaji unaofanywa zaidi na wanawake na vijana na kuwa Tanzania ina kuku milioni 103.1 wakiwemo kuku wa asili na kisasa.
Kupitia Jukwaa hilo, Dkt. Biteko ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzisha mashamba ya kuku wazazi kwa ajili ya kuzalisha vifaranga, kuanzisha vituo vya kisasa, maabara pamoja na kuwekeza katika machinjio ya kisasa ya kuku.
Dkt. Biteko ametoa maagizo mengine ikiwemo “ Wizara iweke pia mfumo wa mnyororo baridi wa usambazaji wa kuku, iwekeze pia katika vizimba, chakula cha kuku na ianzishe viwanda vya kusindika vyakula vya kuku ili vipatikane ndani ya nchi na sio kutumia fedha za kigeni kuagiza nje,”
Ametoa wito kwa wadau wote wa ufugaji wa kuku kuendelea  kushirikiana na Serikali kutekeleza majukumu yao kwa kuwa Serikali  imetoa fursa kwa kila mmoja kuweza kujishughukisha na kujiongezea kipato.
Aidha  Dkt. Biteko ameikaribisha sekta binafsi kushiriki katika tasnia hiyo ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi huku akiwataka watafiti kushirikiana na Serikali.
Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, . Abdallah Ulega amesema  kufanyika kwa mkutano huo ni matokeo ya  mkutano wa AGRA uliofanyika Dar es alaam na kuongozwa na  Rais Dkt. Samia ambapo walielezwa juu ya kuipa kipaumbele sekta ya ufugaji wa kuku kwa kuwa nchini Tanzania familia nyingi zinafuga kuku
“ Tunawashukuru AGRA na Food Alliance kwa kutukubalia na ndio maana leo jukwaa la kwanza limefanyika hapa Tanzania na kutoa fursa kwa wafugaji wetu kujifunza na kujenga mahusiano,” amesema Mhe. Ulega.
Amebainisha kuwa takwimu zinaonesha kuwa ifikapo 2030 kuku watachangia asalimia 41 ya protini na kuwa watafiti nchini washirikiane na Serikali wanapotoa matokeo ili kutoleta taharuki kwa jamii kupitia matokeo ya tafiti zao.
“ Hivi  karibuni watafiti walifanya utafiti kwa kutumia sampuli chache juu ya ulishaji wa kuku wanaofugwa na akina mama na vijana tafiti ile ilileta taharuki, kupitia Jukwaa hili ,”.
“nitumie fursa hii kuwaambia watafiti washirikiane na Wizara ili kutotoa taarifa za taharuki kwa jamii na kuwa Serikali inaweza kudhibiti wafugaji wasiofuata taratibu hivyo tusiharibu jitihada zinazofanywa na kukuza tasnia hii,” amesema  Ulega.
Naye, Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Bodi ya Muungano wa Mapinduzi ya Kijani barani Afrika (AGRA), Dkt. Hailemariam Dessalegn, amesema kuwa fursa muhimu zilizopo kupitia ufugaji wa kuku ni chanzo cha protini, soko la uhakika na ajira kwa vijana na ka kushiriki katika mnyororo wa thamani.
“Jukwaa hili linatoa fursa ya kujifunza faida na changamoto katika tasnia hii na kuongeza ushirikiano. Kukuza tasnia hii katika nchi yetu inahitaji majukwaa kama haya na inahitaji utayari  wa wadau mbalimbali kwa kuwa wana uwezo wa kuwekeza ili kukuza tasnia hii,” amesema  Dessalegn.
Mfugaji kutoka nchini Malawi, Grace Gondwe amesema kuwa baada ya kumaliza Chuo Kikuu nchini humo alianzisha biashara ya ufugaji wa kuku wa kisasa licha ya kukutana na changamoto mbalimbali amemudu kufanya kazi hiyo kwa miaka mitano sasa na kuwa tafiti mbalimbali zinaonesha mahitaji yake yaongezeka siku hadi siku.

You Might Also Like

Watumishi wa Umma Watakiwa Kuwa na Nidhamu, Ubunifu

Mpango Mkakati wa Takwimu wazinduliwa

Tuwaombe Rais Samia, Mwinyi – Sheikh Swed

Biteko Amwakilisha Rais Samia Harambee Ujenzi Kanisa Katoliki

Miradi Ufungaji Mifumo Ya Umeme Jua 20,000 Mbioni Kuanza

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Vijana Wahimizwa Kushiriki Kikamilifu Soko Huru la Afrika
Next Article Rais Samia Akabidhi Tuzo Kwa NSSF Ya Usimamizi,  Uratibu Wa Hifadhi Ya Jamii Kw Sekta Binafsi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?