MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaendesha Warsha Kujenga Ushirikiano Na washirika Wa Maendeleo  
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaendesha Warsha Kujenga Ushirikiano Na washirika Wa Maendeleo  
Habari

Serikali Yaendesha Warsha Kujenga Ushirikiano Na washirika Wa Maendeleo  

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendesha mafunzo ya Washirika wapya wa Maendeleo na Wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyojikita katika kuimarisha uelewa wa taratibu, sera, na mikakati ya maendeleo ya nchi.

Mafunzo hayo yanalenga pia kushirikiana katika utekelezaji wa Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF)  katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Habari Picha 9996

 

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Fedha wakati akifungua warsha hiyo siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam, Kamishina, Idara ya Fedha za Nje, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Zanzibar Yussuf Ibrahim Yussuf amesema kuwa dhamira ya warsha hiyo ni kuhakikisha serikali inaweka ushirikiano madhubuti na Washirika wa Maendeleo.

 

“Serikali zote mbili – ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar – zinaendelea kuimarisha ushirikiano na Washirika wa Maendeleo wenye misingi ya uwazi, uwajibikaji na kulingana na vipaumbele vya taifa. Mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 na Zanzibar 2050,” amesema  Yussuf.

Habari Picha 9997

 

Amesema kuwa warsha hiyo ilikuwa ni pamoja na kutoa uelewa kwa Washirika wapya wa Maendeleo kuhusu mazingira ya kisera, taratibu, na mifumo ya kitaasisi inayosimamia misaada ya maendeleo nchini Tanzania.

 

Yussuf, amesema, Mada zilizowasilishwa na kujadiliwa katika Warsha hiyo ni pamoja na Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF), Mzunguko wa Bajeti ya Serikali, Dira za Maendeleo za 2050, na Mwongozo wa Uandaaji, Utekelezaji na Usimamizi wa Miradi na Majadaliano ya Mikopo, Dhamana na Misaada.

 

Aidha Yussuf amesema kuwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuendena na kasi ya kukua kwa teknolojia kunahitaji ushirikiano wa karibu, upatikanaji na usimamizi wa fedha za mabadiliko ya tabianchi kupitia vitengo maalum vilivyoanzishwa, usimamizi bora wa fedha za umma, ikiwemo kuongeza uwazi na udhibiti wa matumizi ya bajeti.

Habari Picha 9998

 

“Maeneo mengine ya ushirikiano huo ni Maendeleo ya miundombinu, usafiri, nishati, maji na teknolojia za kidijitali. Msaada wa kiufundi katika maeneo ya kidijitali na akili mnemba (AI) kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma na ushindani wa kiuchumi,” amesema  Yussuf

 

Amesema kuwa ufanisi wa ushirikiano wa maendeleo unategemea uwazi, mawasiliano, na uelewa wa pamoja juu ya sera, mipango na miongozo ya kitaifa na juhudi za kuhakikisha Washirika wa Maendeleo wanalinganisha misaada yao na mzunguko wa bajeti na vipaumbele vya taifa.

 

“Tunathamini kwa dhati uhusiano wetu na Washirika wa Maendeleo kwa Mchango wao wa kifedha, kitaalamu na kimawazo ni nguzo ya mafanikio yetu,” ameongeza Kamishina Yussuf.

Habari Picha 9999

 

Mafunzo  hayo ya kujenga uelewa yaliwashirikisha Washirika wa Maendeleo (DPs), Wakurugenzi wa Sera na Mipango (DPPs) wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wakurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti (DPPR) wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

Warsha hiyo imeaandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Fedha za Nje, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za nje na kuhakikisha matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 

You Might Also Like

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030

Nchemba Afungua Mafunzo Ya PAC

Zaidi Ya Wanachama 800 Wa TUGHE Watembelea Hifadhi Ya Mlima Kilimanjaro

Majaliwa Awaagiza Wahandisi Kuzingatia Miiko, Maadili  Ya Taaluma Yao

Tanzania Yaingia Saba Bora Duniani  Kwa Uzalishaji Wa Pamba Hai

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Katibu Mkuu Ahimiza Uzalendo Na Uadilifu Kwa Wanachama wa Ewura CCC
Next Article MOI Kuendesha Kambi Maalum Ya Uchunguzi,  Ushauri Wa Kitabibu Kwa Wazee
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?