Na Danson Kaijage
DODOMA: IMEELEZWA kuwa vijana wabunifu wanaoweza kutengeneza vifaa mbalimbali kama silaha au vifaa ambavyo vinaweza kuonekana hatarishi, wanalindwa kuona ni namna gani vinaweza kutumika.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Tume hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Dkt. Nungu amesema bunifu nyingi ambazo zinafanywa na vijana si kwamba zinazuiliwa lakini zinaangaliwa kwa kuzingatia nini faida kwa maana ya mladi au ni wapi bunifu hiyo itatumiwa.

Akizungumzia vijana ambao wanafanya bunifu lakini inasemekana kuwa wanakamatwa na vyombo vya dola kama kubuni bunduki na vifaa mbalimbali ambavyo ni sehemu hatarishi amesema kuwa kazi ya serikali au vyombo vya dola ni kumpatia ulinzi kwa ajili ya usalama wa mbunifu huyo.
Akizungumzia mafanikio kwa kipindi cha miaka minne, amesema kwa mwaka 2021-2025, Tanzania imeendelea kupiga hatua katika maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
Amesema kwa utashi thabiti wa kisiasa na dira ya kuifanya Tanzania kuwa taifa linalojegwa kwa kutumia sayansi na teknologia, serikali imewekeza ssh. Bilioni 25.7 katika utafiti, ubunifu na maendeleo ya teknolojia kupitia tume hiyo.
Amesema Serikali kupitia COSTECH, imefadhili zaidi ya tafiti 50 katika sekta za Elimu, kilimo, afya, na mazingira ili kuhakikisha maarifa hayo yanatumika kuboresha maisha ya Watanzania.
Na zaidi ya vituo vya ubunifu 111 zimeimarishwa, huku tafiti zikibadilika kuwa suluhisho za kisayansi kwa jamii. Kampuni mpya zipatazo 70 zimesajiliwa ikiwa na matokea ya wabunifu waliyowezeshwa na serikali .
Amesema Serikali imetoa fedha na kuweka mazingira rafiki kwa wanasayansi na wabunifu wa Kitanzania. Kupitia mfumo wa ushirikiano wa kimkakati kati ya serikali ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na taasisi za kimataifa, COSTECH imepokea Sh Bilioni 5.65 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya utafiti wa pamoja kati ya watafiti wa Tanzania na washirika wenza.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, serikali imetenga Sh. Bili 6.3 kwa ajili ya miradi ya utafiti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, huku Shilingi Mil.i 600 zikielekezwa katika miradi minne ya usalama wa chakula, ikihusisha udhibiti wa magonjwa ya mazao,
“Uboreshaji wa uhifadhi wa chakula na ubunifu wa vyakula vyenye virutubishi vya hali ya juu,” amesema