MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Samia Kalamu Award yasogeza Mbele
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Samia Kalamu Award yasogeza Mbele
Uncategorized

Samia Kalamu Award yasogeza Mbele

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read

 

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

CHAMA cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameongeza muda wa maombi ya ushiriki katika Tuzo za Samia Kalamu Awards hadi Oktoba 30, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Dkt. Rose Reuben amesema awali tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ilikuwa Oktoba 26, mwaka huu.

Amesema uamuzi wa kuongeza muda umechukuliwa ili kutoa nafasi kwa wale waliokutana na chagamoto za kiufundi, ikiwemo kushindwa kuipandisha kazi mtandaoni kutokana na matatizo ya mtandao na chagamoto nyingine.

“Tunapenda kuwataarifu waandishi wa habari, vyombo vya habari, maafisa habari na wadau wa habari kuwa muda wa kuomba kushiriki katika tuzo umesogezwa mbele hadi Octoba 30,2024 “amesema

Dkt Rose amesema Tuzo hizo zitatolewa kwa wanahabari wa kitanzania zikiwa na lengo la kuhamasisha, kukuza na kupanua wigo wa uandishi, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani, kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni, ili kuchochea uandishi wa makala za kina zinazozingatia maendeleo.

Aidha amewaomba wale wote ambao awajawasilisha kazi zak kuchukua hatua za haraka na kufanya hivyo kabla kufikia Octoba 30, 2024 .

“Hii ni fursa adhimu kwa vyombo vya habari, waandishi wa habari, maafisa habari kuonesha umahiri wao wa kuchakata habari na kuthaminiwa Kwa michango yao katika taaluma ya uandishi”amesema Dkt Rose

Dkt Rose alisisitiza kuwa kazi zinazowasilishwa zinatakiwa kuwa za kipekee na ambazo hazijawahi kuwasilishwa kuwania tuzo nyingine, na zinazofuata taratibu za haki miliki. Waandishi wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kupitia tovuti rasmi ya www.samiaawards.tz

Kwa upande wa takwimu za maombi ya tuzo Dkt Rose amesema hadi Oktoba 23, mwaka huu wamepokea maombi kutoka mikoa 23 ya Tanzania ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Mtwara, Simiyu, Geita, Njombe, Mbeya, Songwe,Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Kagera, Mjini Magharibi, Ruvuma, Lindi, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro na Pwani.

Vilevile amesema mchakato wa upigaji kura Kwa wananchi inatarajia kuanza rasmi Novemba 8 mwaka huu hivyo aliwahimiza wanahabari kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhim wa kushiriki katika upigaji kura kwa wingi, kwani kura za wananchi zinachangia asilimia 60 ya alama za mshindi, huku asilimia 40 zikiamuliwa na jopo la majaji.

Dkt Rose amesema Wananchi wataweza kupiga kura kupitia namba maalumu ya SMS SHORT CODE 15200 au kwa kutumia tovuti rasmi,”ameswma Dk.Rose.

Kwa upande wake Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Mhandisi Andrew Kisaka amesema tuzo hizo ni muhimu kwa ajili ya kukuza na kutambua mchango wa waandishi wa habari katika masuala mbalimbali yakiwemo ya maendeleo.

“Nawahimiza wanahabari kutoka redioni, televisheni na mitandao ya kijamii kuziwasilisha kwa haraka katika kipindi hiki kilichobaki kwani tunaamini zimeleta mabadiliko chanya kwenye jamii,”amesema Mhandisi Kisaka.

You Might Also Like

Bandari ya Kilwa kuleta mapinduzi sekta ya uvuvi nchini

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

TASU yaiomba serikali inunue meli kutoa ajira kwa mabaharia

Vinasaba 524 Vimepimwa Kwa Mkemia Mkuu

Rais Mwinyi aipongeza Airpay kudhamini tamasha la fahari ya Zanzibar, kusaidia wananchi kupata mikopo kidigitali

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wadau wa Kisekta watakiwa kukabiliana na athari za mvua msimu 2024/25
Next Article Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nishati Safi Kwa Kila Mtanzania Inawezekana – Saidy
Habari August 7, 2025
Bodi ya Maziwa Yatoa Mafunzo ya Ubora, Usalama wa Maziwa Katika Maonyesho ya Nane Nane
Habari August 7, 2025
Balozi wa Tanzania Nchini Italy Afurahishwa  Ubunifu wa TPHPA Maonesho ya Nanenane
Habari August 7, 2025
Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?