Na Mwandishi Wetu
MWANZA: MGOMBEA nafasi ya Rais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 7, 2025, ameendelea na kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa chama hicho katika Mkoa wa Mwanza.
Katika ziara hiyo, Samia amekutana na kuzungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM katika wilaya ya Misungwi, ambapo amesisitiza umuhimu wa mshikamano, amani na maendeleo endelevu kwa Watanzania wote.

Hii ni sehemu ya muendelezo wa mikutano ya kampeni inayoendelea kufanyika nchi nzima kuelekea uchaguzi mkuu ujao.