Na Lucy Ngowi
SINGIDA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete, amekagua maandalizi ya sherehe za sikukuu ya Wafanyakazi ijulikanayo kama Mei Mosi mkoani Singida.
Ridhiwani amesema, “Mapema leo (jana), nimepita Manispaa ya Singida, kuangalia maandalizi ya sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi ( Mei Mosi). Maandalizi yanakwenda vizuri na hatua iliyopo sasa ni zaidi ya Asilimia 88.

“Ninawashukuru sana Viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Katibu Mkuu Henry Mkunda kwa kazi nzuri akishirikiana na uongozi wa Mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendegu,”.
Amesema Mei Mosi itapeleka neema na mabadiliko makubwa Mkoa wa Singida. #KaribuniSingida #MeiMosi2025

.