Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya siku mbili mkoani Mwanza kwa ajili ya
kukagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotaraji kuhitimishwa mkoani hapo Oktoba 14, mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba.
Akiwa Mwanza Ridhiwani amekutana na makundi mbalimbali ili kuhamasisha ushiriki wa kilele hicho na wiki ya Vijana ambayo inaanza Oktoba nane hadi 13.

Ridhiwani katika ziara yake kwenye Viwanja vya Furahisha alikutana na makundi ya vijana wasanii katika fani mbalimbali na baadae kukutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Walimu wa sekondari na vyuo toka wilaya zote za Mkoani humo.
Katika kukutana nao aliwahimiza kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge ikiwa ni pamoja na kushiriki kilele cha wiki ya vijana.
Pia alikwenda Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya halaiki yanayoendelea.