Na Lucy Ngowi
PWANI: MBUNGE wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amewataka
wananchi wajiandikishe ama kuboresha taarifa zao katika Daftari la kudumu la Mpiga Kura ili wachague viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu.
Ridhiwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-anayeshughulikia masuala ya Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu amewataka wananchi hao kujiandikisha, ili wapate nafasi ya kuchagua viongozi baada ya yeye kuboresha taarifa zake.

Amesema wananchi watakapojitokeza kuhakiki taarifa zako, Oktoba mwaka huu watapata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka ili haki muhimu ya kupiga kura isiwapite.
Ridhiwani amehakiki taarifa zake katika Ofisi ya Kata ya Msoga kwa ajili ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zake katika Daftari la kudumu la Mpiga kura ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi.
Uandikishaji huo umeanza Februari 13 mwaka huu, utaisha Februari 19, 2025,.