MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwan Kikwete awaagiza maofisa kazi kushirikiana na WCF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwan Kikwete awaagiza maofisa kazi kushirikiana na WCF
Habari

Ridhiwan Kikwete awaagiza maofisa kazi kushirikiana na WCF

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRIi wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Ridhiwani Kikwete amewaagiza maofisa kazi kote nchini, kushirikiana na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutoa taarifa kwa wakati za wafanyakazi wanaoumia maeneo ya kazi ili waweze kupewa stahiki zao kama Sheria inavyotaka.
Ridhiwan ametoa agizo hilo  jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha siku mbili baina ya WCF na maofisa kazi kutoka mikoa ya Tanzania Bara.
Ridhiwan pia amewaagiza maofisa kazi hao kusimamia sheria za kazi kwa kufanya kaguzi mahala pa kazi ili kuhakikisha waajiri wanatekeleza matakwa ya sheria ya fidia kwa wafanyakazi.
“Jukumu lenu maofisa kazi ni kusikiliza malalamiko na kwa shughuli zinazohusu WCF jukumu lenu ni kuandika na kutoa taarifa WCF,
“Sio kugeuka washauri wa waajiri ili kudhulumu haki za wafanyakazi,”amesema na kuongeza: “andikeni vitu ambavyo mwisho wa siku wafanyakazi watapata haki zao na sio kuandika ili sheria ionekane haifai,” amesema.
Aidha Ridhiwan amewataka maofisa kazi hao kusoma na kuelewa vizuri muswada wa mabadiliko ya sheria ya huduma za jamii, 2024 ambayo inahusu pia mabadiliko katika sheria ya fidia kwa wafanyakazi ili waweze kuwa wasisimamizi wazuri wa sheria hiyo mara baada ya kuwekwa sahihi na  Rais.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt John Mduma amesema kwamba Mfuko umejizatiti katika kuhakikisha huduma zake zinapatikana kupitia mtandao pamoja na kuimarisha ushirikiano na Idara ya Kazi kupitia maofisa kazi hao kwa lengo la kuhakikisha kiwango cha ukidhi wa uzingatiaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi kinaongezeka.
“Kwa sasa huduma zetu kwa zaidi ya asilimia 90 zinapatikana mtandaoni, lakini pia tumekuwa tukishirikiana vizuri na wenzetu wa Idara ya Kazi kupitia maofisa kazi hawa ambao kiukweli ushirikiano huu umesaidia ‘compliance’ kwa upande wetu,” amesema.
Naye Kamishna wa kazi nchini, Suzan Mkangwa amesema Ofisi yake imekuwa ikishirikiana na WCF kuhakikisha malalamiko ya wafanyakazi wanaoumia au kupata ugonjwa unaotokana na kazi zao yanatatuliwa kwa wakati.
Maofisa kazi 78 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara wamehudhuria kikao kazi hicho.

You Might Also Like

OSHA Yatoa Gawio Kwa Serikali Zaidi  Ya Bilioni 10

Simbachawene: Simu za mkononi zinaondoa umakini kwa watumishi wa umma

TFS Yawataka Wananchi Kufuga Nyuki Kuzuia Uharibifu Wa Mazingira

Muhimbili yarejesha tabasamu kwa Karume baada ya miaka 25 ya mateso

DC Twange Apongeza Wananchi Kuchangia Maendeleo 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia aungwa mkono na Tughe, watalii 800 watua Ngorongoro
Next Article Chagueni Viongozi Wanaofaa-Biteko
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?