MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: REA Yatoa Kipaumbele Ujenzi Miradi Ya Nishati Jadidifu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > REA Yatoa Kipaumbele Ujenzi Miradi Ya Nishati Jadidifu
Uncategorized

REA Yatoa Kipaumbele Ujenzi Miradi Ya Nishati Jadidifu

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WAKALA  wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha umeme wa uhakika na kutoa ajira kupitia miradi hiyo.

Hayo yamebainishwa  na Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu kutoka REA,  Advera Mwijage alipotembelea mradi wa Mwenga Hydro unaozalisha umeme wa maji wa megawati nne  uliopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mwijage amesema kuwa, mradi huo umewezeshwa na Serikali kupitia REA kwa kutoa kiasi cha fedha takribani sh bilioni 16.6 ikiwemo sh bilioni 10 ya kuwaunganisha wateja na sh bilioni 6.6 ya utekelezaji wa mradi huo.

“Sisi kama wakala tunaendelea kufadhili hii miradi kwa kuhamasisha na kuwawezesha wanaojenga miradi ili kuendeleza shughuli za kiuchumi nchini,” amesema Mwijage

Vile vile, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fursa kwa wabia wa maendeleo ambao wanaisaidia Serikali katika kutekeleza uzalishaji wa umeme kwenye gridi, kusambazia wananchi na kutoa ajira.

Naye, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mwenga Hydro, Deograsias Massawe amesema mradi huo umewezesha wananchi wa vijiji 32 vya Wilaya ya Mufindi kupata umeme wa uhakika hivyo, kuwawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Ameongeza kuwa, mradi huo umekuwa na faida kwa wajasiriamali kwa kutoa ajira na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ambao umepunguza gharama za uendeshaji shughuli za kiuchumi kutokana na kuachana na matumizi ya mafuta na kuhamia kwenye matumizi ya nishati ya umeme.

Aidha, ameipongeza REA kwa kutoa fedha kiasi cha sh bilioni 16.6 ambazo zimefanya maunganisho kwa wateja zaidi ya 8000 wa majumbani, hospitalini, mashuleni na kwenye vituo vya afya.

Amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi zikiwemo utoaji wa fedha za kuendesha mradi na Sera wezeshi katika nishati jadidifu.

Mradi umeanza uzalishaji rasmi mwaka 2012 katika Wilaya ya Mufindi na umelenga kuongeza wateja wapatao 2,900 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

You Might Also Like

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Rais Mwinyi aipongeza Airpay kudhamini tamasha la fahari ya Zanzibar, kusaidia wananchi kupata mikopo kidigitali

Vinasaba 524 Vimepimwa Kwa Mkemia Mkuu

Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji

TASU yaiomba serikali inunue meli kutoa ajira kwa mabaharia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 
Next Article Mwanachama Wa TALGWU Akutwa Hana Hatia
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mramba Afungua Mafunzo Ya Teknolojia Ya Nishati Jua Kwa Watalaam
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?