MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: REA Yapamba Moto Uhamasishaji Matumizi Ya Umeme
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > REA Yapamba Moto Uhamasishaji Matumizi Ya Umeme
Habari

REA Yapamba Moto Uhamasishaji Matumizi Ya Umeme

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuhamasisha matumizi sahihi na endelevu ya umeme kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na matumizi ya vifaa vya kisasa vya umeme hususan majiko ya umeme ambayo yanatumia kiasi kidogo cha umeme, salama kwa afya za watumiaji na kwa gharama nafuu.
Hayo yamebainishwa na Wataalam wa REA waliofika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutumia fursa ya miradi ya REA inayotekelezwa mkoani Mara.
Akizungumza katika mkutano na wananchi, Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Abdulrazack Mkomi amesema , majiko ya umeme yanalinda afya za watumiaji na ni nafuu kulinganisha na matumizi mengine ya nishati ya mkaa na kuni.
Ameongeza kuwa, ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, REA itaendelea kusambaza kwa wingi majiko ya gesi nchini ikiwa ni sehemu ya kuitangaza na kurahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Naye, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mara, Omary Gwillah amesema kuwa, mkoa wa Mara umeendelea kuwahamasisha wananchi kuunganisha umeme kwenye vitongoji baada ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha utekelezaji wa mradi wa kuunganisha umeme kwenye vijiji vyote nchini.
Gwillah ameongeza kuwa, Serikali imeweka mkazo katika kusambaza umeme kwa watanzania ili kuwa na maendeleo endelevu pamoja na kujenga uchumi imara na kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa gharama nafuu kwa watanzania wote.
“Kufikisha miundombinu ya umeme hadi kwenye vitongoji kumekuwa kipaumbele muhimu katika juhudi za kuboresha uchumi na maisha ya Watanzania. Kupitia uunganishaji umeme, kutachochea ongezeko la viwanda vidogo na vya kati pamoja na kuboresha huduma za afya na elimu,” amesema  Gwillah.

You Might Also Like

Idadi Ya Wagonjwa Wa Magonjwa Yasiyoambukiza Kuongezeka

Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo

Watahiniwa 72 wa kidato cha nne wafutiwa mtihani kwa udanganyifu, kuandika lugha za matusi

TARURA Yatoa Elimu Nane Nane

OCPD Nguzo Kuu ya Utungaji Sheria – Dkt. Ndumbaro

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mawaziri Tanzania Profesa Mkenda, Silaa Mkutanoni Rwanda
Next Article Majaliwa Asisitiza Serikali Itaendelea Kuboresha Mazingira Ya Uwekezaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?