Na Shani Kibwaswali
DODOMA: RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kazi nzuri inayofanya ya kusimamia fedha za wanachama wake vizuri kwani hivi sasa shirika hilo limepanda.
Rais wa TUCTA Nyamhokya ametoa pongezi hizo siku chache baada ya NSSF kueleza mafanikio yake kwa kipindi cha miaka minne cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani.
Amesema anakumbuka miaka mitatu au minne iliyopita walikuwa na taarifa kuwa mfuko huo ulikuwa na Sh. Trilioni 4.8 ambazo walikuwa wamezitolea taarifa, hivyo baada ya kuelezea mafanikio ya sasa thamani ya mfuko huo ni Sh. Trilioni 9.2 ambalo ni ongezeko kubwa kwa zaidi ya aslimia 90.
“Ukiona inakwenda hivyo lazima uangalie ni nini kiasi kilichopelekea hadi thamani ya mfuko ikapanda na kwa kiwango hicho lakini ukitazama unaona ni ongezeko la wanachama na ongezeko la wanachama linatokana na ongezeko la ajira.
“Ongezeko la ajira kwa sasa linatokana na uvutiaji wa wawekezaji unaofanywa na Rais Samia kwa kweli sisi kama Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi tunampongeza Rais sana kwa jinsi ambavyo ameitangaza nchi yetu kwa wawekezaji wamekuja na manufaa,
“Na tunaona sasa ajira zimeongezeka na hatimaye huu mfuko ni kielelezo tosha kwamba sasa walau watanzania walio wengi wako kwenye nafasi za ajira,” amesema.
Kwa upande mwingine amesema kwenye suala la kupungua kwa muda wa kuwalipa wastaafu mafao baada ya kustaafu, sheria zipo wazi na kanuni zake kwamba walau isizidi miezi miwili maana ya siku 60.
“Kwa sasa wanakwenda kwenye wastani wa siku 22 baada ya kustaafu wanachama wanapata mafao yao,” amesema.
Amesema utaratibu wa mfuko huo kwa sasa wanataka kuwalipa wastaafu ndani ya siku moja, kwamba “mstaafu anastaafu leo kesho anapata mafao yake, sisi tunawapongeza na huduma yao tunapongeza sana,”.
Bodi ya mfuko chini ya utendaji wa mkurugenzi masha amefanya kazi kubwa tunawasupoti tutandelea kusimama nao tunashauri wanachama ambao hawajajiunga na mfuko wajiunge wanapotoka kazini watapata faida nyingi sana