Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan, ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini Tanzania, ambaye utendaji wake umekuwa wa mfano.
Samia amepata nafasi hiyo baada ya mtangulizi wake Hayati Rais Dkt. John Magufuli kufariki dunia miaka minne iliyopita.
Baada ya kushika kijiti hicho, Viongozi wengi wanasifu utendaji wake kutokana na uthubutu katika kuliongoza taifa la Tanzania.
Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Godwin Mmbaga anasema Rais Samia amefanya mengi mazuri kwa Taifa letu, ameanza kuwandaa viongozi katika kutekeleza majukumu yao kimaadili na kidhamira hivyo kuwafanya wajiamini na kuweza kutekeleza majukumu yake kwa kasi iliyotarajiwa.
Kada huyo ambaye amepata kuwa Diwani wa CCM katika Kata ya Upanga Magharibi – Ilala na kata ya Lembeni- Mwanga kwa nyakati tofauti na kuwaletea wananchi wake maendeleo mbalimbali yasiyosahaulika ndani ya Kata hizo, amemsifu rais Samia kwa namna alivyotambua kuwa nchi ni Siasa safi, Siasa safi maendeleo na kwamba maendeleo yana watu ila hayana chama.
Anasema hayo yamedhihirika kwa jinsi alivyoweza kusimamia na kutekeleza mifumo yake ya watu kuvumiliana, kukubaliana na kusuluhishana.
Mafanikio ya falsafa hiyo hadhimu barani Afrika yamesababisha kuwe na hali ya uhuru wa kuzungumza, uhuru kulalamika, uhuru wa kutoa habari na uhuru kutekeleza majukumu ya kisiasa bila kukanyagana, kusigina Katiba wala kukiuka sheria za nchi.
Anasema Samia ameweka misingi mizuri na kuvifanya vyama vya siasa kuwa huru na hata kukuza demokrasia katika utendaji wao wa ndani na mengineyo mazuri.
“Hapa tunampongeza kwa kupevusha uendeshaji mfumo wa vyama vingi.
“Ndiyo maana umeona leo hii wanasiasa wamepata sauti za kuzungumza, kuchaguana, kuchambuana na kufurahia siasa na maendeleo ya Taifa.
“Nchi imefunguka tuomeona tija ya maendeleo makubwa ambayo tumeyapata,” anasema.
Jingine alilofanya ni falsafa yake ya kazi iendelee ambayo Mmbaga anasema ameitekeleza kwa vitendo. Mipango yote ya msingi iliyowekwa awali amehakikisha imetekelezwa kwa kiwango kilichotarajiwa na hata zaidi ya matarajio kwa baadhi ya miradi.
Anasema jingine ni namna anavyowajali wananchi bila kuangalia umri wao, jinsia zao wala maeneo walikotoka pamoja na kusimamia kwa makusudi uhuru wa kiuchumi, siasa pamoja na uhuru wa Kitaaluma.
“Tumeona namna alivyobadili uhusiano kati ya walipa kodi na mamlaka za kodi nchini hata kusababisha ongezeko la makusanyo ya kodi pasi Wananchi kushinikizwa. Hapa Watanzania tumetambua kuwa utu ni uchumi” anaeleza.
Anampongeza pia kwa mikakati yake ya kukuza ajira kwa kuvutia wawekezaji kuwekeza nchini.
“Kwa mara ya kwanza Taifa letu limeshuhudia kasi kubwa ya wawekezaji kukimbilia kuwekeza Tanzania.
“Mimi ni kiongozi wa Taasisi ya Japan inafadhiliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara ya Japan( AOTS-Japan) na mimi nimekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Taasisi hiyo (AFAAS) ”
“Mwishoni mwa mwaka jana(2024) tulikuwa Japan katika majukumu yetu ambapo Taasisi hii iliandaa AFRICA-JAPAN investment meeting, Makampuni ya Japan yenye dhamira ya kuwekeza Africa yalikutanishwa na ujumbe toka Tanzania, Egypt, Zambia, Ghana na Kenya.
“Hali hii iliyowashangaza wenzetu ni makampuni mengi walikuwa wakitukimbilia Watanzania zaidi. Ni dhahiri kuwa Mama Samia ameinua sana soko la uwekezaji nchini.” anasema.
Anaeleza kuwa uwezo wa kiongozi wa nchi unapimwa kwa kuangalia miradi ya maendeleo na mambo mengine ambayo yanaleta utulivu wa Taifa.
“Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kuweka bayana kuwa CCM madhubuti itazaa Tanzania Madhubuti, Hivi karibuni tumeshuhudia Mwenyekiti wa CCM, Samia akiongoza CCM kubadili mfumo wa kutafuta viongozi wa nchi kutoka CCM kwa mabadiliko ya katiba.
“Lengo lake lilikuwa kuifanya CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka huu kuendelea kutoa viongozi wenye maadili na sifa nzuri ili serikali ipate uongozi bora zaidi.
“Mama Samia ameunda CCM Madhubuti akidhamiria kujenga Taifa Madhubuti,” anasema.
Mmbaga anaeleza kwamba rais amewaandaa wasaidizi wake kisaiokolojia kujiamini na kutenda kazi kwa uhuru na kuhimiza utendaji unaokidhi matarajio ya Wananchi hapa ndipo akatoa kauli ya “ukinizingua, nitakuzingua” Hapa alimaniisha ukitimiza wajibu wako hakuna atakayekubugudhi, anaeleza Mmbaga
Anasema maandalizi hayo ni pamoja na kuandaa tabia na maadili ya watu, alipiga vita vitendo vya rushwa, upendeleo, ubaguzi, kutokuthamini watu na vingine visivyofaa.
Anasema wakati wote Rais Samia amekuwa akikemea wanaokula rushwa na kubadhili mali za Wananchi.
“Na pale ndipo alipotoa kauli akasema” kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba “ alimanisha kuwa Kila mtu ale kadiri ya stahiki zake kazini