Na Mwandishi Wetu
KILOSA:“NIMPONGEZE sana sana Mhandisi Seff, wataalam na timu yake ndani ya TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya Tanzania nzima, nimemvisha maua yake”.
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi hizo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Victor Seff.
Pongezi hizo amezitoa alipozungumza na wananchi wa Berega wilayani Kilosa mara baada ya kufungua daraja la Berega lililojengwa na TARURA.
Amesema daraja hilo litasaidia kuwaunganisha wananchi lakini kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Pia amewataka wananchi kutunza daraja hilo, kwa kuwasihi wasichimbe mchanga ili liweze kutumika miaka mingi.
“Wananchi mnaharibu mazingira, fanyeni shughuli zenu kwenye mto lakini msiharibu mazingira msichimbe mchanga kwenye mto huu, daraja hili limechukua fedha nyingi ili wananchi mnufaike, tunzeni daraja hili “, amesema.